WAKATI Rais John Magufuli,akisisitiza kuuwajibisha Uongozi
wa eneo lolote nchini kwa uzembe wa Shule kukosa madawati,imeelezwa zaidi ya Wanafunzi 500 wa darasa la kwanza
katika shule ya Msingi Ulowa,Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Wilayani
Kahama,wanaketi chini.
Akiongea na Gazeti hili
Diwani wa Viti Maalumu kutoka katika Kata ya Ulowa,Gabriela Alphonce, alisema mbali na ukosefu huo wa madawati pia kuna
upungufu wa madarasa hali inayolazimu wanafunzi kusomea katika vyumba viwli vilivyotengenezwa
kwa maturubai.
Diwani huyo alisema
mazingira hayo ya shule yanavunja hali wazazi ambao wamekuwa wakijitahidi
kuhakikisha vijana wao wanapata sare nzuri za shule pamoja na Madaftari,hivyo
kuitilia shaka sera ya kupata elimu bure kama itakuwa na ufanisi kwa Taifa .
Aidha alisema kuwa Wanafunzi hao wa Darasa la
kwanza wapo 609 huku wasichana wakiwa 303 na
wavulana 307 na kuongeza kuwa shule hiyo pia ina vyumba vinane tuu vya
madarasa ambavyo vinatumika kwa sasa huku mahitaji halisi yakiwa ni vyumba 25.
Pia Diwani huyo aliendelea
kusema kuwa katika shule ya Msingi Kangeme pia kuna upungufu wa Matundu 62 ya
vyoo huku matundu manne tuu yakitumiwa ma Wanafunzi wa shule hiyo hali ambayo
inafanya Wanafunzi wengine kujisaidia Vichakani.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Ushetu, Isabela Chilumba,katika Kikao cha baraza la Madiwani
,alikiri kuwepo kwa hali hiyo katika shule hizo na kuongeza Halmashauri yake
imejipanga katika kujenga Vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Msingi
Ulowa ili kuweza kupunguza mrundikano wa wanafunzi darasani.
“Kweli Halmashauri yangu
inakiri kuwepo kwa wimbi la Wanafunzi zaidi ya 500 wa darasa la kwanza katika
shule ya Ulowa na hii inatokana na mwitikio wa wazazi kuwapeleka wanafunzi
shule kwa mwaka huu na changamoto inayotukabili sisi kama Halmashauri ni
kuhakikisha kuwa vumba vya madarasa vinajengwa”, Alisema Isabela Chilumba.
Aidha alisema kuwa wazazi
wamejitokeza katika kuwaandikisha wanafunzi elimu ya msingi na kuongeza kuwa
Halmashauri yake haiwezi kuwarudisha wanafunzi majumbani kwa kuwa tayari wazazi
walishaghramika kuwanunulia mahitaji muhimu ya shule Wanafunzi hao.
Aidha aliendelea kusema
kuwa kwa Upande wa Shule ya sekondari Halmashauri yake tayari imeshatatua
changamoto zilizokuwepo ikiwemo upungufu wa madawati hali ambayo tatizo
zilimebaki katika baadhi ya shule za Msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo
mpya.
Rais Magufuli alirejea kauli yake hiyo,wakati akiongea na baadhi ya
wazee wa Dar Es Salaam,kwa kuonya kutowajibika ipasavyo kutasababisha serikali
yake kutoendelea kuwaonea aibu bali itaendela kutumbua majipu .