SERIKALI
ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kutumbua majipu,kadri ya maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,John
Magufuli aliyotoa na kuahidi katika hotuba yake ya kwanza,kwa safari hii Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais{TAMISEMI}
kutengua uteuzi wa Mkurugenzi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais{TAMISEMI},George Simbachawene,ameendeleza utamaduni huo
kwa kuamua kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Tunduma,Halima
Mpita kwa kumsimamisha kazi kutokana na matumizi mabaya ya madaraka.
Mpita
anatuhumiwa kwa upotevu wa mapato ya Serikali,yanayotokana na ushuru wa magari
yanayosafari nje ya nchi kupitia mpaka wa Tunduma sambamba na kuwaingiza kazini
watoto wake kinyume cha sheria na kuwalipa posho.
Baada
ya kutengua uteuzi huo,alimteua,Erick Mapunda,aliyekuwa Mkuu wa Idara ya
Utawala na Rasilimali Watu katika Jiji la Mbeya,kukaimu wadhifa huo.
Mbali
na Mkurugenzi huyo,pia utumbuaji majipu uliwafikia Wakurugenzi watatu wa
Halmashauri za Mbogwe,Misenyi na Nanyumbu sambamba na Ofisa mmoja wa Halmashauri
ya Kilolo,kwa tuhuma za kuwarubuni na kutoa rushwa kwa maofisa wa Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Serikali{CAG},ili hati za Halmashauri zao ziandikwe vizuri.
Waziri
Simbachawene anasema Wakurugenzi hao kwa nyakati tofauti mwaka jana Wakurugenzi
hao walitoa fedha kuwapa maofisa wa CAG,wwakati wakitekeleza wajibu wao wa
kukagua Halmashauri hizo.
Amemtaja,Elizaberth
Kitundu,aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi,Mkoani Kagera,kuhusika
na kufanya jitihada hizo kwa kumtuma Mweka Hazina wake,Majaliwa Biakwaso kutoa
Sh.3 Milioni kwa maofisa wa CAG kusudi wafiche kasoro walizobaini.
Aidha
kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu,mkoani
Mtwara,Alli Kasinge kupitia kwa Mweka Hazina wake,Paschal Malowe na Mhasibu wa
Halmashauri hiyo,Emmanuel Mugesa,walimpatia Fedha kiasi cha Sh.3.5,Ofisa wa
CAG,F.Mwampashi,kwa niaba ya wenzake ili waandike Hati safi.
Katika
Halmashauri ya Mbogwe,Mkurugenzi wake,Abdallah Mfaume na Mweka Hazina
wake,Lucas Elias walitoa Sh.16 Milioni kwa maofisa watatu wa CAG ili kuficha
madhaifu yaliyojitokeza katika Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe,ikiwemo matumizi
mabaya ya fedha kiasi cha Sh.200 zilizofanywa pasipo nyaraka.
Pia
Sh.144 Milioni kulipwa kwa Mkandarasi pasipo kufanyika kazi
iliyokusudiwa,sambamba na kubainika malipo ya Mishahara ya Watumishi 82 kufanyika
huku wakiwa tayari wameishahama katika Halmashauri hiyo.
Kwa
upande wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo,mtumishi wa Idara ya Fedha,Lackson
Pina,alitumia kiasi cha Sh.200,000/= kumpatia Ofisa wa CAG kwa malengo ya
kulinda mapungufu yaliyojitokeza katika Halmashauri hiyo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI