NANI anasema soka la Tanzania halina mvuto ama
ushabiki?Pamoja na Watanzania kubobea katika upenzi wa soka la Uingereza,lakini
ushabiki wa soka la hapa nchini bado una nafasi hasa kwa Watani wa Jadi,Yanga
na Simba.
Pambano la Yanga na Simba
lilikuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa ambapo Yanga iliyokuwa imejificha Kisiwani
Pemba,na Simba mji kasoro bahari,huku likiwaacha mashabiki wake sambamba na
viongozi wao na chembe chembe za hofu,lilimalizika kwa Yanga kuendeleza ubabe
kwa watani zao kwa msimu kwa kuwapachika bao 2 – 0.
Inafahamika kwamba mechi
ya watani hao ni kubwa na yenye ushawishi mkubwa barani Afrika huku ikishikiria
na nafasi ya tatu,na kwa ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa ndio kinara ambapo
imedhihirisha hilo kutokana na ushabiki ulioambatana na utani mkubwa miongoni
mwa mashabiki wa timu hizo.
Utani huo wa jadi ambao
ulionekana kupotea kwa fikra za kutekwa na soka la Uingereza,umeonekana kurejea
kwa kasi kubwa hususani katika Mji Mdogo wa Isaka baada ya mashabiki wa timu
hizo kufanyia utani mara baada ya pambano hilo kukamilika.
Mashabiki hao walioamua
kuketi eneo moja na kushuhudia pambano hilo kupitia king’amuzi cha Azam,baada
ya pambano mashabiki wa Yanga wakiongozwa na Gambalala Daud waliwafanyia utani
wenzao wa Simba kwa kuwanunulia vyakula vyenye rangi za njano na kijani na
kuwakabidhi.
Mbali ya kuwanunulia
vyakula hivyo,pia waliwanunulia soda zilizokuwa za njano na kuwanywesha,kisha
walianza kuwapitisha katika mitaa kadhaa ya Mji huo maarufu kwa jina la Bandari
ya nchi kavu,kisha waliwaongoza hadi katika kaya zao na kuwakabidhi katika
familia wanazomiliki.
![]() |
SHABIKI wa Yanga,Gambalala Daud,mwenye Kibaghalashia,akimkabidhi mboga na matunda shabiki wa Simba,Shija Kinga,akimtaka aanze kula majani kwakuwa hana meno tena ya kutafuna nyama. |
“Ninyi ni wake zetu hivi
vyakula tulivyowanunulia tumetimiza wajibu wetu kama wanaume,chonde chonde
msijifanye vidume kuwashurutisha wake zenu kuvipika,ingieni jikoni ninyi
wenyewe na sasa hivi vipokeeni na kuviingiza ndani,”alisema Gambalala kwa mmoja
wa mashabiki wa Simba,Shija Nkinga ambaye alipokea na kuingiza ndani mwake.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI