Tuesday, February 23, 2016

MWINYI KAZIMOTO APANDISHWA KIZIMBANI NA KUKANA SHITAKA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



MCHEZAJI Nguli wa soka katika timu ya Simba Sport Club,ambayo mwishoni mwa wiki ilipokea kipigo cha bao 2 – 0 kutoka kwa watani zake Dar Yanga African,Mwinyi Kazimoto,amekana shitaka linalomkabili la kumshambulia na kumdhuru mwandishi wa habari za michezo wa hgazeti la Mwanaspoti.

Kazimoto alikana shitaka hilo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Shinyanga mara alipopandishwa kizimbani kwa kosa la kumshammbulia na kumdhuru mwili mwandishi wa    wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Mwanahimba  Richard.

  Akisomewa  shitaka hilo  mahakamani  hapo na mwanasheria  wa serikali,Upendo  Shemkole  alisema mshitakiwa  alitenda  kosa la  shambulizi  la kudhuru  mwili  Februari  10/2016,  katika uwanja wa CCM kambarage   baada  ya  mazoezi  alionekana  kumshambulia  mwandishi  wa  habari  Mwanahimba  Richard.

Hata  hivyo  mshitakiwa  Mwinyi  Kazimoto   baada  ya kusomewa  shitaka hilo  alikana  kutenda  kosa  hilo , na kuiomba  mahakama  kumpatia mwezi   mmoja  ili atafute  wakili  wa  utetezi  wake  ombi  ambalo  lilikubaliwa.

Hakimu mkazi , mfawidi wa  mahakama  hiyo  Rahim  Mushi  anayesikiliza  kesi  hiyo  alisema   imeahirishwa  hadi  March  21  mwaka,  huu  ndipo  itaendelea  tena  kusikilizwa  ili kutoa fursa  kwa mshitakiwa  kupeleka  wakili wake wa utetezi.

Jumla ya mashahidi  sita wanatarajiwa  kutoa  ushahidi  mahakamani hapo katika  kesi hiyo inayomkabili kiungo  mchezaji  wa  Simba  Mwinyi  Kazimoto,  ambapo  pia alipatiwa  dhamana  sh  500,000 na mwanasheria wa halmashauri  ya wilaya ya Shinyanga   Batromeo   Lwela.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI