TUME ya
Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Kaguta Museveni, kuwa mshindi wa
uchaguzi wa urais uliofanyika
Alhamisi hii,hivyo kupata fursa
ya kuendelea kuiongoza Uganda.Akimtangaza Mshindi,Mwenyekiti wa Tume,Dkt.Badru Kiggundu alisema Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa.
Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.
Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.
Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI