Saturday, February 20, 2016

YANGA YAENDELEZA UBABE KWA SIMBA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




MABAO mawili yaliyofungwa na Washambuliaji wa Kimataifa wa Yanga,Donald Ngoma na Amissi Tambwe,yamewawezesha mabingwa hao watetezi kuendeleza ubabe kwa Watani wao wa Jadi katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mabao ya Mabingwa hao watetezi yalipachikwa kimiani mnamo dakika ya 39 ya mchezo na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe,huku bao la pili likifungwa na raia kutoka Burundi,Hamis Tambwe mnamo dakika 72 ya mchezo.

Katika pambano hilo la Watani wa Jadi linaloshikiria rekodi ya tatu Afrika kwa mechi za Mahasimu,likitanguliwa na National Al-Ahaly na Zamaleck za Misri,zinazofuatiwa na Tunis Express na Raja Casabranka za Tunisia,na nafasi ya 20 Duniani,mnamo dakika ya 25,katika faulo ambayo haikuwa kubwa,Mwamuzi wa mchezo, Jonesia Rukiya alimlamba Kadi ya pili ya Njano kisha kumtoa nje kwa Kadi Nyekundu Abdi Banda wa Simba,kwa kumwangusha Ngoma.

Aidha baada ya Mtanange huo,mshambualiaji wa Kimataifa wa Yanga,Amis Tambwe,alisema pambano hilo lilikuwa la ushindani na kilichowponza Simba na kuwa faida kwa tiimu yake ni kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa Banda.


Hata hivyo alisema Simba walijitahidi kucheza vizuri licha ya kuwa pungufu,na kujinasibu kuwa timu yake ya Yanga ilikuwa bora zaidi katika mchezo huo ndio maana imeibuka na Ushindi wa bao 2 -0 kama ilivyokuwa katika mchezo wa kwanza.


Yanga katika mchezo huo iliwakilishwa na Ally Mustapha ‘Barthez’,Juma Abdul,Haji Mwinyi,Pato Ngonyani,Vicent Bossou,Mbuyu Twite,Deus Kaseke{Geofrey Mwashiuya dak 64},Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe,Donald Ngoma na Haruna Niyonzima{ Simon Msuva dak 53}.

Nayo Simba iliwakilishwa na;Vicent Agbani,Hassan Kessy,Mohammed Hussein ‘Tshabalala’,Juuko Murshid,Abdi Bhanda,Justuce Majabvi,Mwinyi Kazimoto{ Novat Lufunga dak 46},Jonas Mkude,Hamisi Kiiza{ Danny Lyanga dak 59},Ibrahim Ajibu{ Bryan Majwega dak 80}
na Said Ndemla.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI