HATIMAYE Watumishi Saba katika Halmashauri ya Mji wa Kahama,waliosimamishwa kazi na wengine kuwekwa katika Uangalizi,kutokana na kutuhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za
ushuru wa huduma, zilizotolewa na Mgodi wa Buzwagi,wamekamatwa na Polisi.
Watumishi
hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Uzabuni katika Halmashauri
hiyo;Marko Nzengula ,hivi karibuni walisimamishwa na wengine kuwekwa
katika uchunguzi baada ya kutuhumiwa kutumia kwa maslahi yao binafsi
kiasi cha zaidi ya
Shilingi Milioni 800,zilizotolewa kwa lengo la
kutekeleza miradi ya wananchi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo ,Anderson Msumba,watumishi hao walikamatwa na Polisi siku ya Jumamosi,baada ya Kampuni ya Noble Cliff Construction likiwa na vielelezo vya kua na nyaraka za kupatiwa kazi na halmashauri hiyo kujitokeza kudai malipo,ilhali yaliishafanyika huku nyaraka zake zikikosa ulinganifu sahihi na nakala ya Bodi ya Uzabuni.
Kufuatia hali hiyo
ilibainika kuwa Bodi ya Zabuni iliipa kazi Kampuni ya
na kuilipa fedha kwa madai ina akaunti katika Benki ya NMB na mkataba yote
ilionyesha fedha hizo zitapitia huko,hali iliyopishana na madai ya Kampuni hiyo
ya kulipwa fedha kupitia Bank Of Africa BOA.
Baada ya kuwepo mpishano
huo wa madai kupishana na mikataba,Msumba alisema alimtuma Mweka hazina wake
kwenda kukagua Akaunti hizo na kukuta ile ya BOA,ambayo Kampuni hiyo ilidai
ilipwe iliishafungwa siku nyingi na ile ya NMB ambayo ilipitishwa na Bodi ya
Zabuni ilikuwa ikimilikiwa na mtu binafsi.
Hali hiyo Msumba alisema
kulikuwa na udanganyifu katika zoezi zima la Mchakato wa utoaji wa zabuni
hiyo,ambao Bodi hiyo ilitoa zabuni za ujenzi mbalimbali kwenye makampuni
hewa,hali iliyosabisha,Mkuu wa Wilaya Vita Kawawa kuunda Kamati ya Uchunguzi
iliyogundua ubadhirifu wa fedha hizo Milioni 800 kati ya Bilioni Moja zilizoko
kwenye thamani ya Miradi hiyo.
Aidha katika tukio hilo la
juzi la kampuni ya Noble Cliff kuonekana ni moja ya makampuni yaliyopewa miradi
hiyo na Bodi hiyo ya Zabuni bila kufuata taratibu,wajumbe wote wa Bodi ya Zabuni
ya Halmashauri ya Mji wa Kahama walikamatwa mpaka kufikia jana walikuwa
Mahabusu katika Kituo kikuu cha wilaya.
Waliokamatwa ni pamoja na
Katibu wa Bodi ya Zabuni,Joseph Maziku,ambaye ni Afisa Ugavi pamoja na Wajumbe
wake Kulwa Ntaudyimara ambaye ni afisa
utumishi,Annastazia Manumbu,ambaye ni Afisa Elimu Sekondari,mwingine
aliyekamatwa ni Joachim Henjewele ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ardhi,Elius Mollel
ambaye ni Afisa Biashara pamoja na Gervas Lugodisha kutoka Ofisi ya Ugavi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Shinyanga Mika Nyange,alikiri kukamatwa kwa watumishi hao na kuongeza kuwa leo
Jumatatu atatoa ufafanuzi zaidi juu ya hatua iliyofikiwa kuhusu tuhuma za
watumishi hao,baada ya kuwasiliana na Mkuu wake wa Polisi wa wilaya ya Kahama
OCD.
Katika tuhuma hizo Mkuu wa
Wilaya ya Kahama,Vita Kawawa,kupitia baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo,ambapo
Mwenyekiti wake Abel Shija aliwasiamamisha kazi watumishi watano kwa tuhuma
hizo kwa kutumia vibaya Fedha za Mgodi wa Buzwagi wengine ambao walikwishahamishwa
aliamua warejeshwe kujibu tuhuma zao.
Na katika tuhuma hizo zilizopelekea
kukamatwa kwa watumishi hao ni baada ya kuanza kupatikana makampuni hewa
yaliyolipwa fedha hizo huku mengine mawili yanaendelea kutafutwa ambayo tayari
kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo yameishalipwa fedha hizo za
Buzwagi.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI