SERIKALI
wilayani Kahama imeshtusushwa na mapato madogo
yanayoingia katika Halmashauri ya Msalala kutoka Mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu,hivyo kuwaagiza madiwani katika Halmashauri hiyo,kufanya utafiti wa
kina kubaini idadi ya makampuni yafanyayo kazi Mgodini,na kustahili kulipa ushuru wa huduma.
kina kubaini idadi ya makampuni yafanyayo kazi Mgodini,na kustahili kulipa ushuru wa huduma.
Agizo hilo alilitoa Mkuu wa wilaya ya
Kahama,Vita Kawawa,katika kikao cha Baraza la Madiwani baada ya Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo,Patrick Karangwa,kueleza matarajio ya kukusanya ushuru wa
huduma kwa mwezi Julai hadi Desemba 2015,kiasi cha Shilingi Bilioni 1.4 kutoka
mgodi huo kadri ilivyokisiwa hawakuyafikia baada ya kukusanya Shilingi Milioni
916.1.
Mkuu
huyo wa wilaya,hakuridhishwa na mapato yanayopatikana kwenye
Halmashuri hiyo kutoka kwa
mwekezaji huyo,na kuwaagiza madiwani waisimamie vyema Halmashauri yao kwa kuona
umuhimu wa kuangalia upya takwimu zote za makampuni yaliyomo
ndani ya mgodi.
“Madiwani
mna dhima kubwa kuishauri serikali na kusimamia mapato ya Halmashuri yenu,msisite
kwenda Mgodini kuyabaini makampuni ili mvune kinachostahili,nami nitakuwa bega
kwa bega kuhakikisha stahili ya Msalala inapatikana kwa kupata ushuru wa huduma
hata kwa kampuni iliyofanya biashara na Mgodi kwa siku moja,”alisema Kawawa.
Kwa upande wake Mbunge
wa jimbo la Msalala,Wilayani Kahama,Ezekiel Maige,aliwataka Wawekezaji wa
Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kuwa wazi kwa
Halmashauri ya Msalala kutoa takwimu halisi ya makampuni wanayofanya nayo
kazi,ili kurahisisha Halmashauri yao kupata stahili sahihi ya ushuru wa huduma.
“Kwa sasa kuna
umuhimu wa Halmashauri ya Msalala, kutengeneza makubaliano baina yao na
Mgodi huo ili kuwa na mikataba ya kudumu,ili Wananchi waweze kujua hali ya kazi
za Wafanyabiashara wanaofanya kazi na Kampuni hiyo,na ili kudhibiti mapato
hayo ni vyema Halmashauri ikawa na ofisi
ndani ya Mgodi,”alisema Maige.
Akiongea kwa Niaba
ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa, Mweka hazina wa
Halmashauri hiyo Deus Ngeranizya alisema kuwa katika Mgodi wa huo wa Acacia
Bulyanhulu kuna jumla ya makampuni 25 yanayofanya kazi katika Mgodi huo hali
ambayo ilipingwa vikali na Madiwani wa Halmashauri hiyo.
Hata hivyo Madiwani
hao walisema kuwa wanataka kujua jumla ya Makampuni yaliopo katika Mgodi huo
ambayo yanafanya kazi na kuongeza kuwa haiwezekani kwa Mgodi wa Acacia
Bulyanhulu kuwa na Makampuni machache kiasi hicho kupita Mgodi wa Buzwagi mbao
ni mdogo wenye jumla ya Makampuni 168 yanayofanya kazi katika Mgaodi huo.
Naye Mwenyekiti wa
Kamati ya Elimu katika Halmashauri ya Msalala Gerald Mwanzia alisema kuwa
Kamati yake iliomba mchanganuo wa fedha hizo kutoka katika uongozi wa Acacia
Bulyanhulu zilizolipwa na Makampuni yanayofanya kazi mgodini hapo lakini
ilishindikana kutokana na uongozi wa Mgodi huo kushindwa kutoa ushirikiano.
Alisema kuwa baada
ya kutopata ushirikiano wa kutosha kutoka Mgodini hapo Kamati hiyo haikuridhika
na majibu pamoja na idadi ya Makampuni inayodaiwa kuwepo katika Mgodi huo ikiwa
ni pamoja na yale yanayofanya kazi katika Bandari ya Nchi kavu ya Isaka ambapo
kuna Makampuni zaidi ya 30.