nguvu katika Kijiji cha Ididi Kata ya Nyamilangano wilayani Kahama.
Kwa mujibu wa Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Shinyanga,Mika Nyange,alisema tukio hilo lilitokea juzi baada ya
Mganga huyo,Jilumba Mabula {70},kuuawa akiwa
katika harakati za kumnywesha dawa,mgonjwa wake huyo,Shibo Joel{20}.
Kamanda Nyange alisema
Joel ambaye ni mkazi wa Kwimba Mkoani Mwanza alifikishwa nyumbani kwa mganga
huyo na ndugu zake akisumbuliwa na
maradhi ya akili na ugonjwa wa kifafa ambapo alipoanza kupewa dawa aligoma
kunywa huku akidai hana ugonjwa wowote.
Aliendelea kusema baada ya
Joel kugoma kunywa dawa kwa madai hana ugonjwa wowote ndipo ilipomlazimu mganga
huyo kuomba msaada wa watu kumshika mtuhumiwa huyo na kuanza kumnywesha kwa
nguvu dawa.
Nyange alisema akiwa katika
hatua hiyo Joel alifyatuka mikononi mwa watu waliokuwa wakimshikilia na
kuchukua jembe la Mkono lililokuwa jirani na walipokuwa na kumpiga nalo sehemu
za shavu la kulia hali iyosababisha Mganga huyo kuvunjika taya na kufariki papohapo.
Aidha Kamanda Nyange,alisema
Joel ameshikiliwa na Polisi mjini Kahama katika mahabusu maalumu,kutokana na
kuhisi anatatizo la akili kwakuwa kwa mujibu wa sheria ugonjwa wake huo
utathibitishwa na daktari baada ya kufikishwa mahakamani .
Baadhi ya watu katika Kata ya Nyamilangano,wamekilaani kitendo hicho na
kwamba kimeacha simanzi kutokana na mganga huyo kuwa msaada mkubwa wa matibabu
mbalimbali mbali na magonjwa ya vichaa kwa kutumia tiba za asili.