Monday, February 8, 2016

VIONGOZI WA DINI WAZIASA MAHAKAMA NCHINI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




VIONGOZI wa dini wilayani Kahama wameziomba Mahakama kutekeleza wajibu wao wa kutoa haki kwa uwazi na
pasipo upendeleo,jambo litakalowafanya wananchi kuwa na imani na chombo hicho hivyo kuwa chachu ya kudumisha amani iliyopo nchini.

Wakiongea juzi katika hitimisho la siku ya Sheria iliyofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya wilaya ya Kahama,viongozi hao wa dini za Kiislamu na Kikristo,walisema nchi nyingi duniani amani zao huvurugika kwa wananchi wake kutopatiwa haki,hivyo kuonya suala hilo lisipewe fursa nchini.

Sheikh wa wilaya {BAKWATA}wilaya ya Kahama,Sheikh Omary Damka,aliwakumbusha Majaji na Mahakimu,kuwa shughuli wanazofanya ni za utumishi wa Mwenyezi Mungu hivyo hawana budi kuwa waadirifu na kuwa majasiri katika kutenda haki kwa kukabiliana na baadhi ya wanaotaka kupindisha sheria kwa ukwasi na mamlaka yao.

“Mwenyezi Mungu amekasimu mamlaka yake duniani kwa viongozi wa dini na serikali,hivyo kwa mnaosimamia sheria mna dhima kubwa ya kutenda haki kwa uadirifu pasina woga wa kuwaogopa wenye kipato ili wasio nacho wasinyanyasike,na hapo mtakuwa mmesimamia amani nchini,”alisema Sheikh Damka.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Anglikana wilayani Kahama,Patrck Kulije,aliwaomba   watumishi wa mahakama  waepuke vishawishi na kuzingatia upendo amabao ndio utakuwa dira ya kutekeleza majukumu yao kwa uadirifu na uwajibikaji uliotukuka hivyo kuwa chachu ya kudumisha amani nchini.

  ambapo alisema TAKUKURU imekuwa chachu ya kuwafanya wafanyakazi wa mahakama kuogopa kuomba na kupokea Rushwa na kusababisha kufanya kazi kwa maadili

Kyaruzi alisema taasisi hiyo ni mdau mkubwa wa Mahakama kwa kuwa nayo inafanya kazi kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo kama itajikita kwa watumishi wa kada zote za mahakama itasaidia kupunguza Rushwa kwa wananchi pamoja na watumishi hao

Alisema taasisi hiyo kama itajikita kwa watumishi hao ana imani itatendeka zaidi na kuongeza kasi ya utendaji kazi ingawa kwa mwaka jana mahakama zote za mwanzo pamoja na ya wilaya zimefanya vizuri kwa kumaliza kesi zote kasoro mahakama mbili tu ambazo nazo ziko  katika hatua ya mwisho kumaliza

Pia kyaruzi alisema katika kipidi cha mwaka jana jumla ya kesi 1118 zilifunguliwa lakini 1105 zimekwisha na bado kesi 13 hali ambayo ni hatua nzuri ya utekelezaji wa agizo la jaji mkuu la kutaka mahakama zote nchini kuanza na kesi sufuri kila mwaka unapoanza

Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Takukuru wa Kahama  Amos Lugomela alisema Taasisi yake haipendi kuona watumishi wanakamatwa kwa kuomba na kupokea rushwa isipokuwa inapenda kuona watumishi wanafanya kazi kwa maadili ya kazi yao bila kuomba Rushwa

Lugomela aliwataka watumishi hao wote kutoka mahakama za Mwanzo na ile ya wilaya kuwatumikia wananchi bila upendeleo wowote kwani kuomba na kupokea Rushwa kwa wananchi masikini wanaohitaji huduma ni dhuluma ambayo haikubaliki kwenye jamii na kwenye maadili ya utendaji kazi za umma

Naye mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa aliwaomba viongozi wa Mahakama Kutenga siku ya kutoe elimu ya Kisheria kwa wananchi wa vijijini ambao wengi wao wamekuwa wakipoteza haki zao kwa kutojua sheria na ndio nafasi inayotumiwa na watu wasiokuwa waaminifu kuwadhulumu mali zao

Kawawa alisema hali ya kutojua sheria kwa wananchi wa vijijini hata watumishi wa Mahakama wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakiitumia kupinda haki kwa maslahi yao hali ambayo kama mahakama zitatoa Elimu kwa wananchi dhuluma za kudhulumiwa haki zao hasa wanawake zitapungua

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI