hiyo,Jecha Salum Jecha kuwa utafanyika uchaguzi wa marudio,kuwa si halali kwakuwa ni maamuzi yake binafsi.
Tamko hilo lilitolewa na makamishina wawili wa ZEC,Nassoro Khamis Mohamed na Ayoub Hamad,jana Jijini Dar Es Salaam walipoongea na vyombo mbalimbali vya habari nchini,ambapo walidai tukio la kufutwa kwa uchaguzi huo lilitanguliwa na matukio kadhaa ambayo yalionyesha wazi kuwa kuna kikundi cha watu ambacho kinamshauri mwenyekiti wa tume hiyo.
Makamishina hao wamejitokeza hadaharani kumpinga Jecha wakati wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa wakipinga kile kinachoendelea visiwani Zanzibar, kwa madai kuwa uchaguzi huo sio halali kulingana na matukio yaliyotokea tangu kufanyika kwa uchaguzi halali wa Oktoba 25 mwaka jana.
Wakizungumza na wanahabari Jijini Dar es salaam makamishna hao, walisema wanapinga kufanyika kwa uchaguzi huo wa marudio kutokana na kuvurugwa kwa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984,tangu tukio la kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana,kutokana na Mwenyekiti wa Tume hiyo kutokuwa na mamlaka ya kisheria kufuta uchaguzi huo pasipo kuwashirikisha makamishna wa tume hiyo.
Walisema sababu nyingine inayowafanya kupinga uchaguzi wa marudio ni kutokana na kukamilika kwa uchaguzi wa mwaka jana ambapo uchaguzi huo ulikuwa umekamilika na baadhi ya washindi wa viti vya uwakilishi na udiwani walishakabidhiwa vyeti vyao na mawakala kusaini kuwa uchaguzi huo hauna kasoro hivyo wanashangaa kuambiwa kuwa uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi zilizopelekea kuubatilisha uchaguzi huo.
Waliongeza kurudiwa kwa uchaguzi huo ambao unatarajiwa kutumia zaidi ya bilioni saba hadi kukamilika kwake ni matumizi mabaya ya rasilimali za taifa kwani uchaguzi Zanzibar ulishafanyika na tayari na kinachoendelea ni mbinu za kuubatilisha uchaguzi huo.
Mmoja wa Makamishina hao Nassoro
Khamis alikiri kuwa Tarehe 26 oktoba mwaka jana, CCM iliikabidhi barua ya malalamiko na kumtaka mwenyekiti na
tume kufuta uchaguzi huo wakati tayari vyeti vya ushindi,viliishatolewa kwa
wahusika na Mwenyekiti aliitisha kikao cha tume na kilichoafikiana kuwa maombi hayo hayakuwa na mashiko hivyo
mchakato uendelee.
Khamis alidai baada ya maamuzi ya
tume, siku iliyofuata Mwenyekiti Jecha hakutokea katika ujumuishaji wa matokeo
kwa siku nzima na ndipo waliposikia kuwa ametangaza kufuta uchaguzi bila
kuwashirikisha wajumbe wengine wa tume hiyo ndipo
ofisi ilipozungukwa na wanajeshi na
kuamuriwa kutofanya lolote huku Jaji Mkuu wa Mahakama ya Zanzibar akikamatwa na kupekwa polisi.
Walisema kuwa kwa matukio kama hayo
wanaamini kuwa tume hiyo imeacha kufanya kazi zake kisheria na sasa inafanya
kazi kisiasa jambo ambalo linampotezea sifa Mwenyekiti wa ZEC kuendelea
kuiongoza tume hiyo,huku wakitoa wito kwa wajumbe wengine ndani ya tume hiyo
kuacha kufuata mkumbo na kuamua kusimamia sheria inavyosema ili kuwapatia Wazanzibar
haki yao ya Kikatiba.