Saturday, January 30, 2016

KAHAMA WAPINGA TBC KUTORUSHA LIVE BUNGE.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Wasanii na Michezo,Nape Nnauye.


BAADHI ya Wakazi wa Kahama,wamepinga vikali kauli aliyotoa Waziri wa  habari, utamaduni, wasanii na michezo,Nape Nnauye, kutaka vikao vya bunge kufanyika bila ya kurushwa moja kwa moja na luninga ya
shirika la utangazaji nchini (TBC);kwa madai ni kuiminya demokrasia na haki ya kufahamu kwa wakati kinachoendelea Bungeni.

Mshauri wa masuala ya Biashara wilayani Kahama,Moses  Mwanakulya,alishangazwa na kauli hiyo ambayo hakubaliani nayo kufuatia TBC kuwa chombo cha umma kinachoendeshwa kwa kodi za Watanzania wa kipato cha chini hivyo haistahili kuchukua maamuzi hayo.

Mwanakulya alisema kwa kauli ya Nape inadhihirisha kuwa serikali ina agenda ya siri,pia haitaki wananchi wake wafahamu kinachoendelea kwa kuogopa wananchi wake kufahamu baadhi ya mambo kutokana na kukabiliwa na changamoto nyingi hasa kwakuwa Rais magufuli aliingia na matumaini makubwa.

“Kuna mambo amabyo serikali inaogopa wananchi wake wasiyajue,lakini ni makosa makubwa kama TBC inasema inazidiwa gharama basi iruhusu mashirika mengine yarushe,kwanini kuwe kuna kikwazo kwa mashirika mengine ilhali Watanzania wanataka wafahamu wawakilishi wao wanasema nini Bungeni?”Alihoji Mwanakulya.

Kwa upande wake mkazi wa Kata ya Majengo,Hassani Kagoma,alisema Serikali ni budi itambue demokrasia ina nafasi yake,hivyo kauli ya Nape ina minya demokrasia na kukiuka Katiba inayotoa nafasi ya uhuru wa kupata habari,na kuiomba kuondokana na kuwa na maamuzi ya kutaka kauli za viongozi zifuatwe pasipo kujali sauti za wananchi.

Aliomba mamlaka zinazomzidi maamuzi Nape zitafakari na kuondoa hoja hoja hiyo ambayo kimsingi inawanyima haki Watanzania,hasa kwakuwa Waziri huyo anaonesha madaraka kumlevya kiasi cha kushindwa kutambua tuko katika zama za dunia kuwa kijiji mimoja hivyo wananchi kuhitaji taarifa na maamuzi ya bunge kuyapata kwa wakati.

Nae Mratibu wa Baraza la Vijana la CHADEMA Wilaya ya Kahama,Elevant Charles,alisema kitendo hicho ni kuwanyima haki Watanzania na kudai kama hoja ni gharama,watambue hicho ni chombo cha umma na hakiendeshwi kibiashara bali kwa kodi za Watanzania,hivyo kuomba serikali ibatilishe maamuzi hayo.

Kwa upande wake Sheikh wa Mtaa wa Kahama,Sheikh Ramadhani Damka,alisema kauli hiyo ikitekelezeka itasababisha wananchi kuwa na mashaka na uadirifu wa serikali kwa kuwanyima haki kwa kutopata baadhi ya vitu moja kwa moja na kuingiwa na hisia kuwa  kuna mambo ambayo wanayaficha.

Sheikh Damka alisema kipindi hiki ni cha utandawazi uliosababisha dunia ipo katika kiganja hivyo kauli hiyo ikitekelezeka itaminya demokrasia nchini,hivyo aliomba uwazi uendelee ili wananchi wafahamu Mwakilishi wao anawawakilisha ipasavyo na wamudu kumkosoa pindi wakimuona anakengeuka maadili ya Kitanzania na kutowajibika kwa kile walichomtuma.

Kufuatia maamuzi hayo ya serikali yalisababisha kuibuka kwa Vurugu kubwa,ndani ya ukumbi wa bunge na kusababisha kundi la polisi wa kutuliza ghasia kuingia ndani ya ukumbi huo na kuwatoa wabunge wa upinzani ambao walikuwa wanapinga.  

WABUNGE wa Upinzani wakitolewa nje na Polisi
Pamoja na Bunge kuahirishwa hadi kikao chake cha jioni,bado hakutokea utulivu mbaya baada ya mwenyekiti Chenge kutangaza kuwa kamati ya uongozi ya bunge imesema ratiba ya kikao cha bunge iendelee kama kawaida,kauli ambayo haikuafikiwa na Wabunge wa Upinzani kiasi cha kuibuka upya tafrani kwa kipindi kirefu ndipo polisi walipoingia ukumbini na kuwatoa nje wabunge wa upinzani.

Kama vile haitoshi hata waandishi wa habari nao walitolewa nje na mkuu wa kitengo cha habari elimu na mawasiliano kwa umma,Owen Mwandumbya, hatua ambayo ili walazimu wanahabari kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Kitendo ambacho baadhi ya wabunge wenye taaluma ya habari wamekilaani kwa madai ya kuzuia kutangaza bunge ni hatua ya mwanzo ya kuua uhuru wa habari nchini na hivyo serikali inabidi kujitazama upya.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI