MKAZI mmoja wa Kijiji cha Mwamandi Kata
ya Mwanase,katika Halmashauri ya Msalala,Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Marashi Lutaja
amefariki Dunia
kisha kuzikwa pamoja na mali zake zote alizokuwa akimiliki katika familia yake,kutokana na mazingira ya kifo chake kuhusishwa na imani za Kishirikina.
kisha kuzikwa pamoja na mali zake zote alizokuwa akimiliki katika familia yake,kutokana na mazingira ya kifo chake kuhusishwa na imani za Kishirikina.
Tukio
hilo limetokea juzi katika kijiji hicho baada ya mwanakijiji huyo Mahushi
Lutaja kufariki na baadaye familia yake kupitisha maadhimio ya kumzika na mali
zake zote yakiwemo makreti ya bia na soda aliyokuwa akiyatumia kwenye baa yake,kwa
imani ya kwamba kifo chake kimetokana na kulogwa nao kuhofia kwamba wakibaki na
mali zake,watakumbwa na mauti.
Kwa
mujibu wa Diwani wa Kata ya Mwanase Samson Masanja, Lutaja baada ya kifo chake
alizikwa na baisikeli 1 vitanda 4 na magodolo yake pamoja na masanduku ya nguo
zake zote na vitu vingine vidogovidogo alivyokuwa akitumia
Pia
Masanja alisema, Lutaja pia alizikwa na makreti ya bia na soda ambayo kabla ya
kifo chake alikuwa akiyatumia kwenye biashara yake ya kuuza vinywaji kwenye
kijiji hicho cha Mwamandi ambapo tukio hilo limehusishwa na imani za
kishirikina
Wakati
akiugua ndugu zake waliamini kwamba ugonjwa huo uliopelekea kifo chake
ulitokana na kulogwa hivyo familia yake iliingiwa na hofu hiyo hasa kutokana na
kuwepo madai ya waganga wa jadi kuamini kwamba ndugu yao alilogwa
Habari
zaidi zinadai katika eneo hilo jamii ya huko inaimani na waganga wa jadi hivyo
hata kifo hicho kutokana na familia ya marehemu kuamini waganga hao iliogopa
kurithi mali za marehemu ambapo baadhi ya wananchi wa eneo hilo walidai kwamba
chanzo cha ndugu hao kuziogopa mali hizo ni ushirikina.
Hata
hivyo ndugu wa marehemu ambaye hakutaka kutaja jina lake,alidai kwa upande wa
pesa marehemu alikuwa ameishakaukiwa na akaunti yake kutokana na kusumbuka
kujitibu kwa tiba za kitaalamu na zile za asili.
Afisa
Mtendaji wa kata hiyo Nicholaus Lusana alisema kuna madai kwamba marehemu
alilogwa kutokana na mali zake kupatikana kwa wizi ama njia zisizo halali hivyo
ndugu zake waliamini kuwa ndugu yao amefariki kwa kulogwa na wenye mali
aliowaibia marehemu
Kufuatia
hali hiyo Lusana alisema Ndugu hao waliamini dawa zilizotumika kumloga ndugu
yao zitawakumba na wao ndio sababu ya kumzika na mali zake zote kwa imani hiyo
ambayo hata hivyo amewaonya wananchi wa eneo hilo kuachana nazo
Pamoja
na hayo Lusana alisema anakwenda kijijini kuzungumza na familia hiyo na baadaye
atatoa taarifa zaidi dhidi ya tukio hilo la aina yake ambalo limewashangaza
wananchi wa wilaya ya Kahama na Jimbo la Msalala.