Friday, January 8, 2016

HUREEE SAMAGOOAAAL....ASHINDA TUZO

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




HATIMAYE kiu ya familia ya soka hapa nchini iliyotokana na ugawaji wa tuzo,imetulia baada ya Mtanzania;Mbwana Ally Samatta,kuwa mwanasoka bora
Afrika,kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara hili.

Katika utoaji huo wa Tuzo hizo za soka zilifanyika jana Jijini Lagos nchini Nigeria na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu katika soka,barani Afrika.


Samatta aliibuka mwanasoka bora kwa kuwashinda Muteba Kadiaba,ambaye ni kipa mkongwe wa TP Mazembe na Bounedjah Baghdad wa Algeria anayekipiga Etoile du Sahel.

Aidha Pierre Aubameyang alifanikiwa kubeba tuzo ya mwanasoka bora Afrika kwa mwaka 2015 na kumpiga kumbo Yaya Toure, aliyewahi kubeba tuzo hiyo mara tatu mfululizo katika kipengele cha tuzo  linalohusisha wanasoka wanaocheza nje ya bara la Afrika.

Aubameyang ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Gabon anakipiga katika kikosi cha Borussia Dortmund.


Yaya anayekipiga anayekipiga katika kikosi cha Man City alishika nafasi hiyo huku nafasi ya pili ikienda kwa Andre Ayew ambaye aliongozana na baba yake, Abeid Pele.

Kwa upande wa mwamuzi bora wa soka mwaka 2015,tuzo ilienda kwa Bakary Papa Gassana wa Gambia,kwa kuwashinda waamuzi wengine mahiri wawili;Alioum wa Cameroon na Ghead Grisha- kutoka Misri.

Watanzania wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu kufanyika kwa tuzo hizo ili Samatta aweke rekodi barani Afrika na kutimiza miongoni mwa ndoto alizonazo mwanasoka huyo.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI