KATIBU wa UMWAPA;Wiliam Matonange. |
BAADHI
ya Wakulima wa zao la Pamba wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga,wameilalamikia
Kampuni ya kununua zao hilo ya Afriasian,kwa
kuwasambazia mbegu za pamba ambazo
wanadai hazioti.
Wakulima
hao,walidai maeneo ambayo yamekumbwa na hali hiyo ni ya vijiji vya
Inolelo,Ndoleji na Buginza vyote vya wilaya ya Kisahapu,ambapo walidai licha
kufuata taratibu zote za kitaalamu juu ya kilimo cha zao hilo katika kulipanda
zao hilo lakini mbegu hizo zimeshindikana kuota.
Mmoja
wa wakulima hao Adriano Pasiano,alisema kutokana na wiki tatu kupita pasipo
kuona dalili ya mbegu hizo kuoota imewatia hofu kuwa watakuwa wamepoteza muda
na nguvu zao pia kuingia katika madeni ya mikopo huku wakishindwa kupata tija
katika zao hilo.Pamoja
na jitihada za gazeti la Tanzania Daima kuwasilana na Meneja wa Afrisian,ili
kujibu malalamiko hayo ya wakulima ambapo kampuni hiyo inahusika na kununua zao
hilo wilayani Kaishapu zilishindikana.
Hata
hivyo Katibu wa Umoja wa Makampuni ya Wanunuzi wa Pamba “UMWAPA”,William
Matonange,akiongea na Mwandishi wa Habari hii kwa njia ya simu,alikiri kupata
malalamiko juu ya Kampuni za KCCL ya wilayani Kahama pamoja na Afrisian kudaiwa
kusambaza zaidi ya tani 100 za mbegu za pamba kwa wakulima zimeshindikana
kuota.
“Baada
ya kupata taarifa za malalamiko hayo,nimeyaagiza Makampuni hayo ambayo ni
wanachama wa UMWAPA kuondoa mara moja mbegu hizo kwa wakulima,na kuwapelekea
zinazostahili ili wamudu kupanda katika kipindi sahihi cha msimu kusudi baadae
wapate tija ya zao hilo,”alisema Matonange.
Matonange
akizungumzia hali hiyo alidai kusababishwa na mbegu hizo kutoandaliwa vyema
sambamba na kuwekewa maji na wakulima kwa kushirikiana na mawakala wa waununuzi
wa zao hilo wasiowaaminifu,hali ambayo kwa makampuni yasiyo makini kukagua na
kuzipima mbegu hizo hujikuta wakizisafirisha na kuwakabidhi wakulima bila kuwa
na uhakika wa kuota ama kutoota.