ALIYEKUWA Mgombea Ubunge wa
Jimbo la Kahama Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo “CHADEMA”
katika uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 25,mwaka huu,James Lembeli,amepinga
matokeo yaliyompa ushindi Mgombea wa Chama Cha Mapinduizi “CCM”Jumanne Kishimba,kwa
kufungua kesi katika Mahakama kuu Kanda ya Shinyanga.
Lembeli akiongoza naWakili
wake,Joachim Hamis kutoka Kampuni ya Mpoki & Associaties Advocates ya
Jijini Dar Es Salaam,alifika katika Mahakama hiyo mjini Shinyanga jana na kukamilisha
taratibu zote za kufungua kesi hiyo kupinga matokeo ya Ubunge yaliyompa ushindi
Jumanne Kishimba katika Uchaguzi Mkuu uliofanyioka Oktoba 25,mwaka huu.
Akiongea na Waandishi wa
Habari mara baada ya kufungua kesi hiyo,Lembeli alizungumzia baadhi ya sababu
zilizomfanya kufungua kesi hiyo ambazo ni pamoja na mgombea wa CCM,Kishimba
kutumia vitendo vya Rushwa wakati wa Kampeni zote bila kuchukuliwa hatua yeyote
licha ya kutoa Rushwa hizo Hadharani.
JAMES Lembeli akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kufungua kesi. |
Aidha katika madai
hayo,Lembeli alisema Kishimba aligawa madaftari yenye picha yake na maandishi
yanayoomba kura kwenye shule zote katika jimbo hilo, wakati wa Kampeni pamoja
na viberti vyenye picha yake kwa wanawake hali ambayo ilikuwa rushwa ya
hadharani.
JAMES Lembeli akiambatana na Wakili wake wakitoka kufungua kesi |
Pia madai mengine Lembeli
alisema Serikali ilitumia nguvu kubwa ya dola kumsaidia Kishimba ili apate ushindi
ikiwa pamoja na kukamatwa kwa mawakala wake usiku wa kuamikia uchaguzi hali
ambayo baadhi ya vituo vya kupigia kura havikupata mawakala haraka,mkapa pale
alipotafuwa wengine wa haraka haraka kwenda kuziba mapengo hayo,ambao hawakuwa na mafunzo ya
uwakala.
Kufuatia hali hiyo Lembeli
amewashitaki watu watatu ambapo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa niaba ya
serikali,msimamizi wa uchaguzi kwa niaba
ya tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Kishimba mwenyewe.
Akizungumzia hali hiyo
katibu wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga,Zakaria Obali,alisema hakuna sehemu yoyote ya kupata haki zaidi ya
Mahakama,hivyo Lembeli yuko sahihi kufungua kesi hiyo,ukweli uweze kubainishwa
kisheria.
JENGO la Mahakama Kuu,Kanda ya Shinyanga. |
Nae Hamis,Wakili
anayemtetea Lembeli,alisema yeye kwa wakati huo hana la kuongea zaidi na
kuongeza kuwa anachojua yeye mahakama itatenda haki kwa kila upande kwa
kuwa ndicho chombo pekee cha kubainisha usahihi wa kila jambo kwa kutafsiri
sheria .
Oktoba 25,mwaka huu
Tanzania ilikuwa na Uchaguzi Mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani ambapo katika Jimbo
la Kahama Mjini Jumanne Kishimba wa CCM aliibuka mshindi kwa kura 47 Elfu huku
mshindani wake James Lembeli wa Chadema akipata kura Elfu 30,ushindi ambao jana
tayari umepingwa Mahakama Kuu.