Wednesday, November 18, 2015

SHEIKH PONDA AACHIWA HURU

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


ponda


MAHAKAMA ya hakimu mkazi Morogoro,imemuachia huru Sheikh Ponda Issa Ponda, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.


Sheikh Ponda aliachiwa na Mahakama hiyo baada ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya miaka miwili kwa kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili,katika hukumu ambayo ilitawaliwa na vilio vya waumini wa dini ya Kiislaamu waliokuwa wamehudhuria  Mahakamani hapo.

 Mara baada ya kuachiwa huru, Sheikh Ponda alisema pamoja na uamuzi huo wa mahakama, amekaa mahabusu kwa muda mrefu kutokana na dhamana yake kuzuiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), hivyo haki yake imechelewa kutolewa.

Alisema ipo haja ya Katiba kufanyiwa marekebisho kwa kupunguza mamlaka ya DPP, yakiwamo ya kuzuia dhamana kwa kuwa yeye alikaa mahabusu ilhali hakuwa hana hatia.

Vilio vya furaha vilisikika kutoka kwa wafuasi wa Sheikh Ponda wakiwamo wanawake baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Mary Moyo kumuachia huru.

Kiongozi huyo wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu aliachiwa huru chini ya kifungu namba 235, cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 marejeo ya mwaka 2002.

Hakimu Moyo alisema upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha kwa namna gani maneno aliyoyatoa Sheikh Ponda, yameumiza imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa.

Wakili Abubakar Salimu ambaye alikuwa akimtetea Sheikh Ponda pia alisema mahakama imechelewa kutoa haki kwa mteja wake, na kwamba muda alioupoteza mahabusu hakuna mtu anayeweza kuulipa.

“Sheikh Ponda amekaa mahabusu kwa miaka miwili na miezi mitatu na katika kipindi hicho amefiwa na mama yake mzazi pamoja na baba mkwe wake, na hivyo kushindwa kuhudhuria mazishi, pia alitenganishwa na familia yake, ifahamike kuwa haki inayocheleweshwa ni sawa na haki inayonyimwa” alisema Wakili Salimu.

Mawakili wa Serikali, Sunday Hyera na George Mbalasa wao walisema kwa nyakati tofauti kuwa hawana cha kuzungumza, kwani tayari kesi imemalizika na mahakama imetoa maamuzi.

Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo saa 2:30 asubuhi, akisindikizwa na polisi na askari wa kikosi maalumu cha Magereza waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi.

Kiongozi huyo alionekana akijiamini na aliposhuka kwenye gari alikuwa mwenye furaha na baadaye alianza kusoma gazeti.

Wafuasi wachache wa Ponda waliruhusiwa kuingia ndani ya mahakama hiyo, huku wengine wakizuiwa nje ya uzio kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa ni za kiusalama na kuifanya mahakama iwe katika utulivu.

Mashtaka
Awali, ilidaiwa na upande wa mashtaka kuwa Agosti 10, 2013 saa 12.45 jioni Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege mkoani Morogoro, Sheikh Ponda alikaidi amri halali ya mahakama, kutoa maneno yenye kuumiza imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa. Mashtaka ambayo aliyakana.

Hata hivyo, shtaka la kwanza na kutotii amri ya mahakama liliondolewa mahakamani hapo, baada ya Sheikh Ponda kushinda rufaa na hivyo kubaki na mashtaka mawili.

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi tisa pamoja na vielelezo saba, ikiwamo kamera ambayo ilimrekodi Sheikh Ponda alipokuwa akitenda makosa hayo wakati upande wa utetezi ulikuwa na shahidi mmoja.

Wafuasi wa Sheikhe Ponda wakiangua kilio eneo la msikiti wa dini moja Mungu mmoja kiwanja cha ndege Manispaa ya Morogoro.http://jumamtanda.blogspot.com/http://jumamtanda.blogspot.com/
 http://jumamtanda.blogspot.com/
Mfuasi wa Sheikhe Ponda Issa Ponda akiangua kilio baada ya Sheikh huyo kuacchiwa huru mahakama ya hakimu mkazi Morogoro.
 http://jumamtanda.blogspot.com/ 
Sheikh Ponda akiomba dua katika msikiti wa dini moja mungu mmoja kiwanja cha ndege Manispaa ya Morogoro.
http://jumamtanda.blogspot.com/Mmoja wa wakili wa Sheikhe Ponda Issa Ponda, Abubakari Salim akizungumza na Sheikhe Ponda muda mfupi kabla ya kusomwa kwa hukumu iliyosomwa na hakimu mkazi mahakama ya Morogoro, Marry Moyo leo mkoani Morogoro
http://jumamtanda.blogspot.com/
Wakili msomi Betholomeo Tarimo akizungumza jambo na Sheikh Ponda baada ya kuachiwa huru mahakamani hapo.
http://jumamtanda.blogspot.com/
Sheikhe Ponda akifurahia jambo mbele ya askari magereza wakati wakimpongeza kwa kuachiwa huru.
http://jumamtanda.blogspot.com/
Sheikhe Ponda Issa Ponda akisoma gazeti la Mwananchi muda mfupi kabla ya kusoma kwa hukumu yake kisha kuachiliwa huru katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro.
http://jumamtanda.blogspot.com/


Sheikhe Ponda Issa Ponda akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya hukumu yake ambayo hakimu mkazi mahakama ya Morogoro, Mary Moyo ilimuona hana hatia na kumwachia huru.

http://jumamtanda.blogspot.com/
Sheikh Rajabu Katimba akiwa na Sheikh Ponda 
http://jumamtanda.blogspot.com/
Askari Polisi wakiwa nje ya mahakama ya hakimu mkazi mara baada ya Sheikh Ponda Issa Ponda kuachiwa huru.
http://jumamtanda.blogspot.com/
Sheikh Rajabu Katimba akiwa na Sheikh Ponda (wenye kanzu) waakitoka msikiti wa dini moja mungu mmoja uliopo Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro ambapo sheikh Ponda alizungumza na waumini wa dini ya kiiislam kwa mchango wao.
 http://jumamtanda.blogspot.com/

http://jumamtanda.blogspot.com/
Sheikh  Sheikh Ponda (katikati) akiwa katika gari wakati akielekea katika msikiti wa dini moja mungu mmoja uliopo Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro ambapo sheikh Ponda alizungumza na waumini wa dini ya kiiislam kwa mchango wao kisha kuombewa dua njema katika msikiti huo.
http://jumamtanda.blogspot.com/

Askari wa jeshi la polisi wakiwa wameimalisha ulinzi nje ya mahakama ya hakimu mkazi Morogoro wakati huku ya sheikhe Ponda Issa Ponda ikisomwa.
 http://jumamtanda.blogspot.com/
.PICHA ZOTE KWA NIABA YA MTANDA BLOG.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI