RAIS
wa awamu ya tano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr.John Pombe
Magufuli,anatarajiwa wakati wowote kufanya uteuzi wa Watanzania wenye sifa
stahili za
kuwa Wabunge.
Rais
Dr.Magufuli,atafanya uteuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977,inayompa mamlaka ya kuteua miongoni mwa wananchi,wabunge
wasiozidi kumi,ambao wanaweza kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu katika
sekta za Afya,Elimu,Kilimo,Nishati na Sheria.
Ibara
ya 66{1}inasema,bila kuathiri masharti mengine ya Ibara hii,kutakuwa na aina
zifuatazo za Wabunge,yaani{e}wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka
miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa Ibara ya 67,isipokuwa sifa
iliyotajwa katika Ibara ya 67{1}{b}.
Kufuatia
mamlaka hayo aliyokasimiwa Rais na katiba,baadhi ya Watanzania wana shauku
kubwa ya kuona uteuzi wake kama utafuata nyayo za mtangulizi wake,Rais Mstaafu
Jakaya Kikwete.
Katika
muhula wa pili wa utawala wake,Rais Kikwete,aliteua wabunge kumi,kati yao mmoja
akiwa kutoka chama cha upinzani,kitendo kilichotafsiriwa kuwa alijali kukomoza
demokrasia nchini,kupitia mamlaka yake kwa kuona umuhimu wa mtu kwa Taifa na si
Chama.
Alimteua
Mwenyekiti wa NCCR – Mageuzi,James Mbatia,ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
huu ameshinda Ubunge Jimbo la Vunjo,ni mbunge mteule.
Aidha
katika uteuzi wake ule,kati yao sita aliwapa Wizara za kuongoza,utaratibu ambao
hapana shaka Dr.Magufuli atautumia kulingana na mahitaji ya Serikali,lakini
shauku kubwa ni kuona suala la demokrasia atalipa umuhimu katika uteuzi huo ama
mapenzi ya chama yatamuongoza zaidi na kuutosa upinzani?
Katika
uteuzi wake Rais mstaafu,Kikwete,kwanza alimteua Profesa Makame
Mbarawa,akamfanya Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia;na Shamsi Vuai
Nahodha,aliyepewa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Zakhia
Meghji,aliteuliwa lakini hakupewa wizara yoyote,baada ya kufanya mabadiliko ya
Baraza la Mawaziri mwaka 2012,Rais Kikwete aliwateua Profesa Sospeter
Muhongo{sasa mbunge mteule wa Butiama},akampa Wizara ya Nishati na Madini;Saada
Mkuya na Janet Mbene,akawafanya Manaibu katika Wizara ya Fedha.
Hata
hivyo Janet baadaye aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,ni
mbunge mteule Jimbo la Ileje,Mkuya anasubiri hatima yake Jimbo la
Kijitoupele,Zanzibar.
Uteuzi
wa Rais Kikwete,ulimuona Dk.Asha Rose Migiro kuwa Waziri wa Katiba na Sheria,na
ulikoma kwa kuwateua Dk.Grace Puja na Innocent Sebba,ambao hawakupewa wizara
yoyote.