Saturday, November 14, 2015

LOWASSA KUUNGURUMA LEO ARUSHA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



ALIYEKUWA mgombea wa urais wa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa pamoja na viongozi wanaounda vyama vya Umoja wa Katiba “UKAWA” leo wanatarajiwa kupanda
jukwaani,kumuombea kura mgombea wa ubunge wa Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema.


Mgombea Ubunge katika Jimbo hilo,Lema,katika mkutano wake wa uzinduzi wa kampeni,uliofanyika Soko Kuu juzi, alisema Lowassa atatumia mkutano huo wa kampeni kuzungumza na Watanzania,kuwashukuru kwa kumpatia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliopita.


Awali akizungumza katika mkutano huo,mbunge mteule wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alieleza kuwa Lowassa na viongozi wa vyama vyenye ushirika wa Umoja wa Katiba “UKAWA”,watatoa tamko zito,hivyo kuwaomba wakazi wa Arusha na Watanzania kutega masikio.


Lema ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwataka wakazi wa Arusha, kutokatishwa tamaa na kuendelea kuwa na huzuni kutokana na matokeo ya urais yaliyotangazwa na kuwa bado kuna harakati za chama hicho kusaka haki.


“Ndugu zangu msikate tamaa, tumesikia wengine wametupa shahada zao, hapana, kazi ndiyo imeanza na lolote linaweza kutokea kwa uwezo wa Mungu,” alisema.


Alisema huzuni ya matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), haipo kwa wananchi tu, bali hata wajumbe wote wa kamati kuu.


“...Kwenye kikao cha kamati kuu, kuna wajumbe walimuomba Lowassa atoe tamko... kama angetoa tamko la kupinga matokeo na kukubali watu kuingia mitaani, Tanzania ingekuwa imeingia katika machafuko makubwa.


“Tunaendelea kutumia taasisi za kimataifa kudai haki, ndiyo sababu mnaona Zanzibar wameshindwa kujitangazia matokeo, hii ni kazi kubwa ya Ukawa,” alisema.


Katika mkutano huo, Lema alieleza njama alizosema zinapangwa kumnyima ushindi na akaonya kuwa hatakuwa tayari kuona ameshinda lakini mwingine akatangazwa kushinda.


“Najua Arusha nitashinda kwa kura nyingi, lakini kama wakitaka kunipora ushindi sitakubali,” alisema Lema.


Aliwaomba wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi Desemba 13 kumpigia kura nyingi, ili pia kuwezesha Chadema kupata viti viwili zaidi vya wabunge wa viti maalumu.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI