Tuesday, November 17, 2015

WALIODAIWA KUFA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI MACHIMBONI KWA SIKU 41 WAOKOLEWA WAKIWA HAI.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MMOJA wa Wachimbaji hao,Amosi Mhangwa{25}
WACHIMBAJI sita wa machimbo madogo ya Dhahabu ya Nyangalata wilayani Kahama ambao Oktoba 5,mwaka huu,walidaiwa kufa kwa kufukiwa na kifusi,juzi usiku
waliokolewa wakiwa hai huku hali zao zikiwa mbaya baada ya kuishi  ardhini kwa siku 41.
Akiongea kwa tabu mmoja wa wachimbaji hao,Chacha Wambura{54},ambaye pamoja na wenzake wamelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama,alisema baada ya kukatika kwa kifusi hicho kiliziba njia ya kutokea,na kuwalazimu  kujificha kwenye kona ya mashimo hayo.
Wambura alisema katika machimbo hayo huchimba maeneo ya uwazi kwa ajili ya kuhifadhi vifaa vyao vya kazi ndiko walikojificha na kujinusuru na uhai wao kwa kutopandwa na vifusi na waliishi kwa kula chura,wadudu kama mende,mijusi na ambao waliamini hawana sumu ya kuwdhuru pamoja na mizizi,magome ya miti na kunywa maji.
.

BAADHI ya Wachimbaji hao wakiwa wamelazwa Hospitali Kahama.
.
 Wambura alisema walikikutwa na maafa hayo yeye na wenziwe watano,baada ya kuwaokoa wachimbaji wenzaao na walimudu kwenda katika moja ya vyumba hivyo ndani ya mashimo hayo na kuanza kutafuta njia ya kutokea wakitumia mwanga wa tochi na simu zao za mkononi kabla hazijaishiwa moto.
Hata hivyo awali wakati tukio hilo likitokea Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mgodi huo uliotitia wa Shigomico,Hamza Tandiko,alidai ufukuaji wa eneo hilo ulihitaji gharama kubwa kutokana na kuwa wamefukiwa umbali wa zaidi ya mita 100.
Tandiko alisema kutokana na gharama kuwa kubwa iliwalazimu kuanza mkakati mpya kwa kushirikiana na serikali kuwafukua watu hao ambao tayari familia zao walizitangazia msiba kutokana na kuhisi waliishapoteza uhai wao.
Hata hivyo wakati Serikali ikiwa na mkakati huo wa kuwatoa kwa kufukua eneo hilo kule chini waathirika hao walikuwa wakifanya juhudi binafsi za kujiokoa kwa kupenyeza katika maeneo mengine yaliyoingiliana kule chini ya ardhi.
CHACHA Wambura akiwa amelazwa kwa matibabu zaidi.
Wambura alisema baada ya kuona hali hiyo waliendelea kutafuta njia ya kutokea lakini baada ya siku saba matumaini yalianza kuisha kutokana na wao kuanza kuchoka na pia njaa iliwakaba kiasi cha kuishiwa nguvu na kubaki kutegemea kudra za Mwenyezi Mungu.    
Pia alisema baada ya hapo wakiwa huko chini,waliona Mwanga lakini ukiwa umezibwa na jiwe kubwa hali ambayo ilizidi kuwakatisha tamaa ya kutoka,ingawa sasa kuna eneo waliona chemic hemi ya maji yakitiririka,nakutumia kofia ngumu kukinga na kunywana na kipindi chote walishirikiana kuokoa uhai wao.
Alizidi kufafanua kuwa katika mashimo kuna miti inayofungwa kama nguzo ya kushikilia ukuta wa Shimo,ambayo  walikuwa wakiyabandua maganda yake na kuchimba kiini chake cha ndani na kula,huku wakati mwingine wakikamata wadudu kama vile Mende  na kula.
Kwa masikitiko alimtaja  mwenzao mmoja,Mussa Supana ambaye  aligoma kula aina hiyo ya chakula hali iiliyosababisha siku kumi na tano kabla hawajaokolewa apoteze maisha yake,na wakati huo hali ya uhai kwaoilikuwa ngumu kutokana na vifaa walivyotumia kupata mwanga kama simu betri zake kuisha chaji.
Aidha alisema kuna siku walisikia sauti za wachimbaji wengine wakiendelea na uchimbaji kwenye mashimo mengine kule chini lakini walipopiga kelele ya kuomba msaada watu hao waliondoka moja kwa moja hadi alipotokea huyo mmoja ambaye walijibizana nae na kuwaaahidi kuwasaidia.
Baada ya muda ndipo waliposikia milio ya sauti ya wachimbaji wakitoboa njia mpaka kuwafikia walipokuwa na ikawa sasa wameokolewa ingawa mmoja wao tayari alikuwa amekwisha fariki lakini waliwaeleza hali hiyo ya mwenzao huyo,kufariki.
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Joseph Ngowi,alithibitisha kuwapokea watu hao, Chacha Wambura,Amosi Mhangwa{25},Joseph Bulule Rhobi{44},Msafiri Gelard na Onyiwa Moris {55}na kudai wanaendelea na jitihada za kuokoa uhai wao.
Ngowi alisema hali zao zinaendelea vizuri ingawa kwa sasa hawawezi kula chakula kutokana na utumbo wao kusinyaa,huku nuru za macho yao yakiwa hafifu kutokan na kuishi muda mrefu gizani .
Ngowi alisema kwa kawaida mtu akiishi bila kula chochote na akiwa na afya nzuri anaweza kufa ndani ya siku 14,lakini hawa wamedumu kwa siku 41 kutokana na kula chakula kisicho halisi huku hali ya lishe mwili ilikwisha na walikuwa wakiishi kwa lishe ya protini ya misuli.
Pia Ngowi alisema watu hao hali zao zakawaida zinaweza zikarejea baada ya siku saba kutokana na kuwa chini ya uangalizi wa wataalamu mbalimbali wakiwemo wa lishe, mazoezi ya viungo na saikolojia.
Kwa upande wake Kaimu Kamishina wa Madini Tanzania,Ally Samaje,alisema tukio hilo limewakuta wakiwa safarini kwenda kwenye machimbo hayo kwa lengo la kutaka kulifukua eneo hilo,na kuwaomba wachimbaji wadogowadogo wazingatie taratibu za usalama pindi wanapokuwa katika shughuli za uchimbaji kwa ajili ya kupata dhahabu na kuuza kwa lengo la kupata fedha peke yake.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI