Sunday, October 4, 2015

BREAKING NEWS.. MCH. CHRISTOPHER MTIKILA AFARIKI DUNIA KWA AJARI.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MCHUNGAJI Christopher Mtikila enzi za uhai wake.


HABARI  mpasuko zilizotufikia hivi punde,zinaeleza Mwenyekiti wa Chama cha DP nchini Tanzania, mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia,kutokana na
ajali ya gari.

Taarifa kwa mujibu wa chanzo chetu zinaeleza,Mchungaji Mtikila amefikwa na mauti hayo asubuhi hii Majira ya saa 12 kasorobo Kijiji cha Msolwa karibu na mji wa Chalinze takribani kilomita 15 hivi kutoka Chalinze barabara ya Morogoro mkoani Pwani.

GARI alilokuwemo Mchangaji Mtikila.


Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Jafar Ibrahim amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wengine watatu waliokuwa katika gari hilo wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.


"Kwa maelezo ya dereva,gari ndogo aina ya Salon waliyokuwa wanasafiria iliacha njia wakiwa wanaelekea jijini Dar es salaam,ikapinduka,ilikuwa na watu wanne akiwemo dereva na mchungaji Mtikila,hawa watatu ni majeruhi na mchungaji Mtikila inasemekana amefariki,mwili wa marehemu na majeruhi wako njia wakielekea hospitali ya Tumbi",amesema Kamanda Ibrahim.


Amesema bado wanachunguza chanzo cha ajali hiyo...

Mtikila alitangaza kugombea Urais kupitia chama chake cha DP lakini chama chake ni moja ya vyama ambavyo vilikatwa kutokana na kutotimiza vigezo vilivyokuwa vinatakiwa.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI