WATU
11 wamelazwa katika Kituo cha Afya Lunguya na wengine 11 wakidaiwa uhai wao
kuwa mashakani kutokana na kufukiwa na vifusi vya udongo katika machimbo ya
Nyangarata yaliyopo Kata ya Lunguya katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Nyangarata yaliyopo Kata ya Lunguya katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kwa
mujibu wa Makamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala na Diwani aliyemaliza
muda wake katika Kata ya Lunguya,Benedicto Manuari,alisema watu hao 11
wamelazwa baada ya kuokolewa katika mashimo yaliyo katika machimbo madogo
yaliyodidimia wakati watu hao wakiendelea na shughuli zao za uchimbaji wanaendelea
kupata matibabu katika kituo cha afya Lunguya.
Alisema
kuwa sasa Jitihada zinafanyika za kuwaokoa Wachimbaji hao,baada ya kufanya
mawasiliano na Mgodi wa Dhahabu wa
Acacia Bulyanhulu,kuwapatia kikosi cha uokoaji ili kuweza kuwapata wachimbaji hao walio hai ambao wapo mashimoni wakiendelea
kuwasiliana na wenzao kwa simu za viganjani wakiomba msaada wa kunusuriwa uhai
wao.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Justus Kamugisha alithibitisha kuwepo kwa tukio
hilo lilitokea juzi majira ya saa tatu asubuhi baada ya watu hao 11
kuokolewa kwenye kifusi kilichokuwa kimewafunika katika mashimo waliokuwa
wakichimba Dhahabu huku ikidaiwa wachimbaji hao walikuwa zaidi ya 20.
Kamugisha
alifafanua kuwa tukio hilo lilitokeaa mara mfululizo kwa siku moja ambapo tukio
la kwanza lilitokea majira ya saa tatu asubuhi na lile pili likitokea
majira sita mchana,huku akidai kuna wachimbaji ambao hawajaokolewa wakiwa ndani
ya mashimo hayo na kuongeza kuwa pindi wenzao wanapofanya mawasiliano nao kwa
njia ya simu za mkononi , simu zao zimekuwa zikiita hali inayoashiria kuwa bado
kuna watu.
Kwa
upande wake Afisa Madini Mkazi wa Wilaya
ya Kahama Sophia Omary alipotakiwa kuzungumzia kuhusu tukio hilo alisema kuwa yupo
njiani kuelekea eneo la tukio,pindi akifika na kuoana uhalisia na kujiridhisha
ndipo atakuwa na ushahidi wa kuzungumzia juu ya tukio hilo.