CHAMA
cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini leo kimezindua rasmi kampeni
zake za Uchaguzi mkuu ujao katika viwanja vya Shycom mjini
Shinyanga,ambapo
wabunge wa majimbo yote ya Shinyanga wamehudhuria uzinduzi huo .
wabunge wa majimbo yote ya Shinyanga wamehudhuria uzinduzi huo .
Uzinduzi
huo umeongozwa na waziri wa Uchukuzi mheshimiwa Samweli Sitta na mbunge
wa Mtella aliyemaliza muda wake Livingstone Lusinde ambao walitumia
fursa hiyo kumnadi mgombea urais wa CCM Dkt John Magufuli na kumponda
mheshimiwa Edward Lowassa wakidai kuwa hafai kuwa rais kutokana ufisadi
wake na kwamba Ukawa wamekurupuka kwani hawamjui vizuri Lowassa.
Makada
hao wa CCM pia walisema Lowassa hana lolote zaidi ya mbwembwe na
visingizio vya hapa na pale.
Wanachama wa CCM na wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa CCM katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga leo
Mjumbe
wa NEC taifa Gasper Kileo akizungumza katika mkutano huo ambazo
aliwataka wanaccm kuwapuuza watu wanaozusha kuwa atahamia Chadema/Ukawa
kutokana na kile kinachotajwa kuwa ni rafiki yake na Lowassa,ambapo
Kileo alisisitiza kuwa hajawahi na wala hafikiria kuhama CCM na kwamba
CCM lazima ishinde katika uchaguzi mkuu ujao
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM wilaya ya Shinyanga mjini
Mheshimiwa
Samweli Sitta akizungumza katika mkutano huo,ambapo aliwatambulisha
wagombea ubunge majimbo yote 6 ya uchaguzi mkoa wa Shinyanga ambayo ni
Ushetu,Msalala,Kahama mjini,Kishapu,Shinyanga mjini,Kishapu na Solwa na
kusisitiza kuwa lazima CCM ishinde katika majimbo hayo.
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal akiwasalimia
wakazi wa Shinyanga na kuwaomba wananchi kuchagua wagombea wa CCM kwani
ndiyo watawaletea maendeleo
Mbunge
wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akiwasalimia wakazi wa
Shinyanga ambapo aliwaomba wananchi kuwapa kura wagombea wa CCM
Mgombea
ubunge jimbo la Msalala mheshimiwa Ezekiel Maige akiwasalimia wakazi wa
Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi CCM wilaya ya
Shinyanga mjini katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Mgombea ubunge jimbo jipya la Ushetu mheshimiwa Elius Kwandikwa
akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo ajigamba kuwa katika jimbo lake
wameshamaliza kufanya uchaguzi wanachosubiri ni utaratibu tu tarehe 25
Oktoba mwaka huu.
Mgombea
ubunge wa jimbo la Kishapu mheshimiwa Suleiman Nchambi akizungumza na
wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wanaShinyanga kuwapa kura wagombea
wa CCM kwani ndiyo watakaowaletea maendeleo watanzania
Mgombea
ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza
na wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wakazi wa Shinyanga kutochagua
mbunge ambaye siyo mzawa wa Shinyanga na badala yake wampe yeye kura ili
kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga huku akijisifu kuwa amefanya
mambo mengi ya kimaendeleo kwa wananchi katika sekta mbalimbali kama
vile afya,elimu,michezo n.k
Mheshimiwa
Samweli Sitta akiwahutubia wakazi wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa
kampeni za uchaguzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini ambapo alisisitiza
kuwa mgombea urais wa UKAWA Edward Lowassa anahusika na sakata la
Richmond na utajiri wake haueleweki
Msanii wa nyimbo za asili Madebe Jinasa akitoa burudani wakati wa
uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za Chama Cha Mapinduzi wilaya ya
Shinyanga mjini
Wafuasi wa CCM na wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa CCM leo mjini Shinyanga
Mkutano unaendelea
Mkutano unaendelea
Mheshimiwa
Livingstone Lusinde akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alitumia
muda mwingi kumponda mgombea urais kupitia Ukawa Edward Lowassa hasa
kuhusu afya yake kwamba ni mgonjwa bila kutaja ugonjwa
anaougua/anaoumwa
Mheshimiwa
Lusinde akiwaombea kura wagombea wa CCM na kumpa sifa kem kem
mheshimiwa John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea urais kupitia CCM
Mkutano unaendelea
Mheshimiwa Lusinde akiwahutubia wakazi wa Shinyanga
Tunafuatilia kinachoendelea hapa.....
Mheshimiwa
Lusinde akiwa na wagombea ubunge majimbo yote ya Shinyanga,ambapo mmoja
pekee wa jimbo la Solwa mheshimiwa Ahmed Salum hakuwepo kwenye mkutano
huo kutokana na kuwa katika shughuli zingine za kichama
Wabunge watarajiwa majimbo ya Shinyanga wakiwa jukwaani

Wa tatu kutoka kushoto ni mgombea ubunge jimbo la Kahama mjini mheshimiwa Jumanne Kishimba
Wanachama wa CCM wakicheza uwanjani
Baada ya mkutano kila mmoja akaendelea na shughuli zake wengine wakapanda kwenye magari yao kurudi makwao
CHANZO CHA HABARI Malunde 1 Blog
CHANZO CHA HABARI Malunde 1 Blog