MWEZESHAJI katika semina hiyo,Franuel Reuben. |
inaweza kusababisha kuchagua viongozi wasio na sifa, sambamba na uchungu wa kutetea rasilimali za Taifa.
BAADHI ya washiriki katika semina hiyo. |
Mzuka
alisema wanawake wamekuwa wakirubuniwa kwa kupewa rushwa hali ambayo wamekuwa
wakitumika kama daraja la kujipatia madaraka katika chaguzi mbalimbali huku
wakishindwa kujitokeza kuwania nafasi za uwakilishi kwa kuhofia kuombwa rushwa
ya ngono.
“Wanawake
wanashindwa kujitokeza kuwania nafasi za uwakilishi kutokana na kutokuwa na
pesa za kuhonga kwa viongozi wa vyama vya siasa ili viwapitishe,na kibaya zaidi
pia hutumika kuhongwa khanga,sukari na chumvi ili kupitisha viongozi wabovu
katika chaguzi ambao utumishi wao hujali maslahi yao kuliko ya umma,”Alisema
Mzuka.
MKUU wa Takukuru wilayani Kahama,Enock Ngailo. |
Kwa
upande wake Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani
Kahama,Enock Ngailo,alisema wanawake wanapaswa kutopokea rushwa kutoka kwa
wagombea,vinginevyo watakuwa wanajinyima haki zao za msingi za kuchagua
kiongozi mwenye maslahi na umma.
Aliongeza
kuwa ili mwanamke aweze kupata maendeleo kwenye jamii ni lazima achague
kiongozi mtetezi wa maslahi ya umma,ambaye hakupatikana kwa njia ya Rushwa,na
mwenye uwezo wa kukemea suala hilo kwenye jamii inayosababisha watu wengi
kukosa haki zao.
MSHIRIKI katika semina hiyo,Paul Ntelya,akichangia mada. |
Nae
mwakilishi wa mkuu wa Polisi wilaya ya Kahama,Dismas Kifunde,aliwataka wanawake
kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama pindi wanapoona viashiria vya uvunjifu
wa amani,ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za Kisheria.
SHDEPHA+
inatekeleza mradi huo,unaoratibiwa na OXFAM Ireland na kufadhiliwa na UKAIDS
kutoka Uingereza na USAIDS ya Marekani,ikiwa na lengo la kujadili na kuzipatia
ufumbuzi changamoto zinazowakabili wanawake katika harakati za kuwania
uwakilishi na upigaji kura.