Sunday, August 30, 2015

KLABU YA MAZOEZI YA SKAUTI WILAYANI KAHAMA YAZINDULIWA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

KAMISHNA wa Skauti Mkoa wa Shinyanga,Mussa Chama akiongea.


CHANGAMOTO kubwa inayosababisha hamasa ya Skauti kupungua,ni kutokana na Serikali za wilaya kutotoa kipaumbele
kwa watenda kazi wa vikundi vya skauti kwa kuhakikisha wanawatengea bajeti,sambamba na wazazi kuwazuia vijana wao kwa madai huteswa kwa kupewa adhabu mbalimbali.

MZAZI Chacha Marwa akitoa neno.


Hayo yalielezwa na Kamishna wa Skauti Mkoa wa Shinyanga,Mussa Chama,wakati wa uzinduzi wa Klabu ya Mazoezi ya Skauti wilayani Kahama,ambapo hakusita kueleza jinsi serikali ilivyowatelekeza watendaji kazi wa Skauti kwa kushindwa kuwapangia bajeti huku wakitambua umuhimu wa kambi za Skauti.

VIJANA wa Skauti wakiimba kwa pamoja.


Alisema kuwepo kwa skauti kunasaidia kutoa mafunzo ya uzalendo kwa vijana,hivyo kuwajengea maadili mema ya Kitanzania na kuwaepusha kujiunga na vikundi visivyofaa ambavyo vimekuwa kichocheo cha vijana wengi kujitumbukiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.

VIJANA wa Skauti wakiimba.


Kamishina huyo wa skauti,alisema wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa mazingira magumu kutokana na kutokuwa na mafungu ya kuwaweka mara kwa mara kambini vijana ili kuwapatia stadi za kazi na kuwajengea uzalendo wa taifa vijana.

VIJANA wa Skauti wakicheza muziki.



“Skauti imesahaulika wakati ndio kichocheo kikubwa cha vijana kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya,kwa kupatiwa mafunzo yenye maadili mema,na mioyo ya kujitolea katika shughuli mbalimbali ili kujenga uzalendo wa Taifa letu,”Alisema Kamishina Chama.



VIJANA wa Skauti wa Kike wakicheza.


Aidha alisema kulikuwa na umuhimu wa Serikali kuzielekeza Halmashauri kupanga bajeti kwa ajili ya Skauti,hali itakayowarahisishia watendaji wake kuwaweka mara kwa mara vijana kambini na kuwajengea uzalendo wa kulipenda taifa.

MABINTI wakionyesha umahiri wa kucheza muziki.


Hata hivyo Chama alisema mbali na serikali kuwasahau wamekuwa wakitafuta ufadhili kwa wafanyabiashara ili kuwaweka vijana kambini,lakini wamekuwa wakipata vikwazo kwa baadhi ya wazazi ama walezi ambao wamekuwa na hisia tofauti na masuala ya Skauti.

FARAJA Isack,akisoma risala.


Alisema wazazi na walezi wamekuwa wakizuia vijana wao kujiunga na kambi za skauti kwa imani kuwa watakumbana na mateso kutokana na adhabu wanazopatiwa pasipo kutambua lengo la kambi hizo ni kuwajengea vijana  ukakamavu sambamba na kuwajengea nidhamu njema.

BAADHI ya wazazi na walezi waliohudhuria uzinduzi.



“Maisha ya skauti yanatawaliwa na uzingatiaji wa nidhamu,pamoja na stadi zinazowajenga vijana kuishi katika mazingira yoyote yale huku wakiwa na mioyo ya kizalendo kwa Taifa na si vinginevyo,”Alisema Chama.

MAMA Simba akijiandaa kufungua shampeni ya Uzinduzi.


Kwa upande  wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Felix Kimario,aliwapongeza Skauti  kutokana na kuwa mstari wa mbele katika shughuli mbalimbali za kujitolea katika jamii.


Alisema kambi za Skauti ni muhimu kuendelea kuwepo kwa ajili ya kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwa  vijana,kwa kuwaweka vijana pamoja  kubadilishana mawazo na kelekezana maadili ya Kitanzania,hivyo kuwaasa wazazi kuwahamasisha vijana wao kujiunga na Skauti.




KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI