Monday, August 3, 2015

MIUNDO MBINU YA UMEME INAATHIRI TAALUMA KISHIMBA SEKONDARI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MENEJA wa Atlas Copco,Tawi la Mwanza;Menas Ngonyani,akizindua Maktaba ya Shule ya Sekondari ya Kishimba,Pembeni yake ni Mkuu wa Shule hiyo,Melkisedeck Choya. IMEELEZWA kuwa Shule ya Sekondari ya Kishimba katika Halmashauri ya Mji wa Kahama,inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya Umeme,na kuathiri ufanisi wa Shule hiyo.
WAKIKAGUA Maktaba.
Hayo yalielezwa na Mkuu wa Shule hiyo,Melkisedeck Choya,alipokuwa akisoma risala katika uzinduzi wa maktaba ya shule hiyo,ambapo alikiri kwa kipindi kirefu ufanisi wa kitaaluma shuleni hapo unakabiliwa na kukosekana kwa umeme sambamba na kutokuwepo kwa maabara.

KWAYA ya Shule ikitumbuiza katika hafla hiyo fupi.

Choya alisema pamoja na kuwezeshwa kuwa sekondari ya kwana katika Halmashauri ya Mji wa Kahama,kuwa na Maktaba itakayosaidia kuongeza taaluma kwa wanafunzi kwa kwenda kujisomea na kuazima vitabu vya kiada na ziada,lakini ukosefu wa miundo mbinu ya umeme utaendelea kuathiri ufanisi katika shule hiyo.
MENEJA wa Atlas Copco tawi la Mwanza,Menas Ngonyani,akimpatia zawadi ya Mwamvuli mwanafunzi wa Kidato cha kwanza,Fatuma Miraji,kutokana  na jitihada anazozionyesha katika masomo zinazoambatana na nidhamu na maadili mema.


Alisema mbali na miundo mbinu ya Umeme,pia upungufu wa viwanja vya michezo katika shule hiyo kunaathiri kuibua vipaji vya vijana katika sekta hiyo ambayo katika karne hii inazalisha ajira,huku akisema kuwepo kwa maktaba hiyo kutaongeza ufaulu kwa vijana shuleni hapo.
MENEJA wa Atlas Copco,Tawi la Mwanza,Menas Ngonyani akizungumza na wanafunzi .

“Kwa kipindi kirefu tangu kuanzishwa kwa shule hii hatukuwa na Maktaba,jambo liliofanya walimu wafanye kazi ya ziada ili kuhahakisha wanafunzi wanafyanya vizuri katika mitihani yao,lakini sasa tumerahisishiwa kuwepo kwa maktaba hii,tutaitumia vizuri walimu pia wanafunzi ili kuhakikisha shuleni yetu inafanya vyema katika mitihani ya taifa,”Alisema Choya.
IGIZO la Wanafunzi.
Kwa upande wake Meneja wa Atlas Copco,Tawi la Mwanza,Menas Ngonyani,alisema kampuni yake ambayo inafanya kazi katika Kanda ya ziwa tangu mwaka 2008,imeona irejeshe pato wanalozalisha kwa kusaidia huduma za jamii katika sekta mbalimbali.
MWANAFUNZI wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari ya Kishimba,Fatma Miraji,akifurahia zawadi yake.
Aidha aliwaomba walimu katika shule hiyo kuitumia maktaba hiyo kwa kuanzisha timu za masomo mbalimbali kwa wanafunzi ili kuleta ushindani wa kitaaluma utakaosaidia kufanya vyema kwa wanafunzi katika shule hiyo.

BAADHI ya Wanafunzi wakiwa Maktaba.
Nae mzazi Asha Ally Salmu,aliwasihi wanafunzi katika shule hiyo wasijinyanyapae kwa kuona wanasoma katika shule za Serikali ambazo zinadharauliwa tofauti na zile za “English Medium”,kwa kuwaeleza jitihada na umakini wa kuwasikiliza vyema walimu wao ndio itakuwa dira ya mafanikio yao katika masomo.
MWALIMU Prosper Donard,akielekeza wanafunzi.

“Msihadaike na wanaosoma shule za English Medium,Yes …No ni ileile,cha msingi muwe makini katika kuwasikiliza walimu wenu na kuzingatia maadili ya uanafunzi na shule,mtafanya vyema kuliko hata waliopelekwa hizo shule za Pesa,”Alisema Asha.




MKUU wa Shule ya Sekondari ya Kishimba,Melkisedeck Ngonyani,akisoma Risala.
Maktaba katika shule hiyo imekarabatiwa na Shirika la Read International chini ya ufadhili wa Atlas Copco,na kugharimu kiasi cha Shilingi Milioni Nane,kwa kuhusisha upakaji rangi,kutengeneza kabati za kuhifadhi vitabu,meza na viti sambamba na vitabu vya kiada na ziada. 



























KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI