![]() |
JAMES Lembeli akibebwa kama Mfalme. |
ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Kahama,James
Lembeli,kupitia Chama cha Mapinduzi “CCM” ambaye hivi karibuni ametangaza
kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo,jana
alipokelewa na umati mkubwa wa watu
Mjini Kahama huku akibebwa Kifalme.BODABODA katika mapokezi ya Lembeli. |
Mapokezi hayo ambayo hayajapata kutokea
kufanyika kwa kiongozi wa aina yeyote wilayani Kahama,yalianzia mji mdogo wa
Tinde kilometa zipatazo 38 kutoka mji wa Kahama na kuingia mjini majira ya saa
9:30,yaliongozwa na bodaboda zaidi ya 100,bajaji na magari yalisimamisha
shughuli za kiuchumi katika mji wa Kahama kwa masaa matatu.
BODABODA wakiongoza msafara wa mapokezi ya Lembeli. |
Katika msafara huo wananchi hao walifunga barabara
zote za mji wa Kahama hali iliyosababisha magari kusimama kuunga foleni ndefu
mpaka walipofika kwenye viwanja vya CDT ambapo mkutano huo mkubwa ulifanyika,ukiongozwa
na Wabunge waliomaliza muda wao wa Majimbo ya mkoani Mwanza,Highness Kiwia na
Ezekia Wenje sambamba na Mbunge wa Biharamulo,Athony Mbassa.
JAMES Lembeli alipokuwa akiingia mjini Kahama. |
Wakiwa katika mkutano huo Katibu wa Chadema Mkoa
wa Shinyanga, Zacharia Thomas,alimwelezea Lembeli kuwa ni mwanasiasa
aliyekomaa,mpenda haki lakini kuwepo kwake CCM,kulikuwa sawa na kuifukia nyota
yake jalalani ambapo itang’ara maradufu baada ya kujiunga CHADEMA.
WATU wenye miraba minne wakimbeba Kifalme Lembeli. |
Akiongea katika mkutano wa hadhara,mbunge wa
Jimbo la Ilemela,Kiwia aliwataka wananchi wa Kahama pamoja na kumuunga mkono
Lembeli, wanapaswa kuwa na nguvu ya pamoja pindi akipita katika kura za maoni
za CHADEMA kwa kuhakikisha wanapiga na kulinda kura ili kudhibiti wizi wa kura
ambao unawezwa kufanywa na wasimamizi wa uchaguzi.
UMATI wa watu uliohudhuria mapokezi ya James Lembeli. |
Alisema Lembeli anaweza kushinda kwa kura nyingi
katika Jimbo la Kahama mjini, lakini anaweza kuhujumiwa na wasimamizi wa
uchaguzi ambao ni Wakurugenzi wa halmashauri hali ambayo alisema wasimamie kwa
nguvu ushindi wake.
JAMES Lembeli katika muonekano wa CHADEMA |
Kwa upande wake Lembeli aliyekuwa ameambatana na
mama yake Mzazi, Maria Kasembo, alisema uamuzi alioufanya ulikuwa ni mgumu
lakini wizi na rushwa iliyokuwa ikifanyika katika ofisi za CCM ilimlazimu
kuamua uamuzi mgumu wa kuhama na kujiunga na CHADEMA.
UMATI wa watu katika Mkutano wa Hadhara |
JAMES Lembeli akianza hotuba kwa kusoma Biblia. |
Alisema kuhama kwake CCM na kwenda chadema
atafanya kazi kubwa ya kutetea wanyonge kuliko alivyokuwa akitetea akiwa ndani
ya CCM sehemu iliyojaa wizi na rushwa.
JAMES Lembeli akifuta chozi lililombubujika ghafla. |
Hata hivyo alipofikia kueleza kilichomtoa CCM
Lembeli aliangua kilio akisema pamoja na kufanya kazi kubwa hakupewa shukurani
badala yake akawa mtu wa kuletewa wala rushwa na watoa rushwa ili wagombee
ubunge kwenye jimbo lake la Kahama.
LEMBELI akiongea na umati wa watu katika viwanja vya CDT |
Aidha alisema CCM imenuka rushwa hasa katika
ngazi ya Wilaya ili uweze kukubalika kugombea ni lazima utoe rushwa kwa
viongozi wa juu wa CCM Wilaya hali ambayo alipingana nayo na kuonekana ni
msaliti ndani ya chama.
LEMBELI akifafanua jambo |
Pia alisema pamoja na kugombea ubunge jimbo la
Kahama Mjini kama atashinda na kuwa mbunge atasaidia wananchi wote wa Majimbo
ya Kahama na Ushetu jimbo ambalo limezaliwa kutoka Kahama ambayo kwa pamoja
ameyatumikia kwa miaka 9 na nusu anajua matatizo ya wananchi wote wa majimbo
hayo
Nae mbunge wa jimbo la Nyamagana aliyemaliza
muda wake Wenje alisema anamtambua Lembeli hata alipokuwa mbungeni misimamo
yake ilionyesha kama mpinzani hivyo kuhama kwake CCM huko alikokuja ndiko
atakavyofanya kazi vizuri
SEHEMU ya umati uliomlaki Lembeli. |
Wenje alisema Chadema hakuna mgeni mwanachama
yeyote akiingia leo anaanza kazi hapo hapo hivyo Lembeli tangu siki
aliyoingia alianza kazi siku hiyo na ndiyo maana alikwenda Bunda kufanya kazi
za chama hivyo Kahama wamuunge mkono.
ya kadamnasi.
Kwa kutumia
mkutano huo Lembeli
alitangaza rasmi kuwania ubunge jimbo la Kahama mji na kuwatoa wasiwasi
wagombea wengine wa chama chake kipya kuwa demokrasia itazingatiwa wakati wa
mchakato wa kura za maoni ndani ya chama ili kupata mgombea stahiki na atakuwa
tayari kumuunga mkono kada yeyote wa Chama hicho atakayeteuliwa kupeperusha
bendera ya CHADEMA.
|