Tuesday, July 14, 2015

NEC YATANGAZA MAJIMBO MAPYA 26 YA UCHAGUZI

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MWENYEKITI wa NEC;Jaji Damian Lubuva.

WAKATI Joto la Uchaguzi nchini likipamba moto,Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezidi kuongeza mhemko kwa kutangaza majimbo mapya ya uchaguzi 26,ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kukata kwa majimbo hayo wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia  katika majimbo mapya.
 

Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.


Mengine ni majimbo ya Kondoa Mjini, Newala Mjini, Bunda Mjini, Mbulu Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini, Mbagala, Kibamba,Vwawa,Monongo,Mlimba, Pamoja na Uliambulu.

Jaji Lubuva amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakiingia katika Halmashauri mbili hiyo kuweka mipaka katika maeneo ili mbunge aweze kushiriki katika Halmashauri moja tu.

Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI