BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO
 |
MKURUGENZI wa Shdepha+,wilayani Kahama,Venance Mzuka. |
WAKATI Taifa likielekea
katika Uchaguzi Mkuu,jamii imetakiwa kuchagua viongozi kutokana na uwezo na si
kuangalia jinsi,sambamba na wanawake kushauriwa kujitokeza kuwania nafasi za
kuchaguliwa ili wawakilishe wananchi kwa kujiamini.
 |
MJUMBE katika Mdahalo,Mama Baranoga. |
Mwito huo ulitolewa na
Mkurugenzi wa Miradi Shdepha+,Kanda ya Ziwa,Venance Mzuka,katika Mdahalo wa
siku moja uliohusisha vikundi vya Wajasiriamali wa Kata ya Nyasubi katika
Halmashauri ya Mji wa Kahama,ambapo aliwahamasisha wanawake kujitokeza kuwania
Ubunge na Udiwani.
 |
MWEZESHAJI katika Mdahalo huo,Rajab Thomas. |
Mzuka aliviomba vyama vya
siasa kutoa kipaumbele kwa wanawake ambao wataonyesha nia ya kutaka kuwakilisha
wananchi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,mwaka huu ilimradi wawe wamekidhi
vigezo vya kuwa wagombea sahihi.
 |
MSHIRIKI katika Mdahalo;Munge Kuhoka kutoka Kahama Artistic and Entertaiment Group. |
Nae Afisa Miradi wa
Shdepha+ wilayani Kahama,Rajab Thomas,aliwaomba wanawake waondokane na hofu ya
mfumo dume ya kujiona stahili yao ni kuchagua wawikilishi kwa kupiga kura huku
wakisubiri uteuzi wa viti maalumu.
 |
MWEZESHAJI Rajab Thomas,akiongea na washiriki wa Mdahalo. |
Thomas alisema Shirika
lake linatekeleza Mradi wa Fahamu,Ongea na Sikilizwa ambao unaratibiwa na
Shirika la OXFAM Tanzania baada ya Kupata ufadhili kutoka OXFAM Ireand wenye
lengo la kuwahamasisha na kuwatia ujasiri wanawake watambue haki ya
kujiandikisha,kupiga kura na kuchaguliwa.
 |
MSHIRIKI katika Mdahalo;Samson Kabiligi. |
Hata hivyo Thomas alisema
japokuwa mradi umelenga zaidi wanawake lakini abadani hauwezi kufanikiwa pasipo
kumhusisha mwanaume,ambaye katika kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi anawajibu
mkubwa wa kumtia ujasiri mwanamke ili ashiriki kikamilifu katika uchaguzi.
 |
WASHIRIKI wa Mdahalo katika mjadala wa Vikundi. |
Alisema wanawake wasijione
duni bali watambue wanawajibu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa mwaka
huu kwa kujitokeza kwa wingi kuwania Ubunge na Udiwani na kuondokana na kawaida
yao ya kusubiri kudra ya viti maalum.
Aidha aliwaomba wananchi
wawapime wanawake watakoajitokeza kwa vigezo na si kwa jinsi,kusudi wamudu
kuingia katika vikao vya maamuzi na kutetea stahiki zao na za jamii kwa
ujumla,huku akiwataka wanawake kutokatishana tamaa pindi miongoni mwao
atajitokeza kuwania Udiwani ama Ubunge.
 |
MMOJA wa Maafisa wa SHDEPHA + |
Mmoja wa Washiriki
hao,Mwalimu Luhumbika Japani,alitia shaka kujitokeza kwa wingi wanawake katika
nafasi za Ubunge na Udiwani,kutokana na kutokuwepo kwa elimu ya Uraia
inayostahili kwa jamii kuona umuhimu wa zoezi la kujiandikisha,kupiga kura na
kujitokeza kuwania uongozi.
 |
WASHIRIKI wa Mdahalo. |
 |
WASHIRIKI wa Mdahalo wakijaza fomu. |
 |
KAIMU Afisa Mtendaji kata ya Nyasubi akihitimisha Mdahalo.
Shinyanga,Shinyanga Vijijini na Kahama
mji ili kuwajengea uelewa kwa jamii katika muktadha mzima umuhimu wa
kujiandikisha,kupiga kura na kuchagua ama kuchaguliwa uli kuleta usawa wa jinsi
katika vikao vya maamuzi.
|
Mwalimu Japani alisema
uduni wa elimu ya uraia inaweza kuchangia kutokuwepo kwa mwamko mkubwa wa
wanawake kujitokeza kuwania nafasi hizo za uwakilishi sambamba na kupiga kura.
SHDEPHA+ inatekeleza mradi
huo katika Halmashauri za Manispaa ya
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI