Saturday, July 18, 2015

MGEJA AJITOSA KUWANIA UBUNGE SHINYANGA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MJUMBE wa Baraza la Vijana na Mhamasishaji Vijana Kata ya Nyanhembe wilayani Kahama,Sinzo Khamis Mgeja,kulia,
akichukua fomu ya kuwania Ubunge Viti Maalum kundi la 
Vijana mkoa wa Shinyanga.



MAKAMU wa Rais wa Chuo cha Mtakatifu Maria,Sinzo Khamis Mgeja,ambaye ana taaluma ya Ualimu,amejitokeza
kuchukua fomu za Ubunge mkoani Shinyanga.

Sinzo ambaye ni Mtoto wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa "NEC",Khamis Mgeja,alifika jana majira ya asubuhi katika ofisi za CCM mkoa wa Shinyanga kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania ubunge wa viti maalumu kundi la Vijana mkoa wa Shinyanga.

SINZO Khamis Mgeja ambaye ni Makamu wa Rais wa Chuo cha Mtakatifu Maria,akionesha fomu ya kuwania Ubunge kupitia Kundi la Vijana wa CCM,Mkoa wa Shinyanga. 
Sinzo Khamis Mgeja ambaye baba yake mzazi ni mtoto wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,alichukua fomu hizo na kuzijaza kisha majira ya mchana,kuzirejesha baada ya kufuata taratibu zote zinazotakiwa.

KATIBU wa UVCCM Teddy Athumani,kushoto, akimkabidhi Sinzo Khamis Mgeja fomu ya kuwania ubunge wa viti maalum kundi la vijana mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi,lengo likiwa ni kuwakilisha vijana wa mkoa wa Shinyanga.

Akiongea mara baada ya kurejesha fomu hizo,binti Mgeja,alisema endapo atapata ridhaa ya kuongoza mkoa huo atahakikisha vijana wa Mkoa wa Shinyanga,anawatetea kwa nguvu zote kusudi wafike katika matarajio yao pindi chama chake kikimridhia kupata wadhifa huo.

 
PICHA ZAIDI YA TUKIO HILO;






 
Sinzo Khamis Mgeja,majira ya mchana,akirudisha fomu ya 
kugombea ubunge viti Maalumu kundi la Vijana mkoa wa 
Shinyanga,kushoto ni katibu muhtasi ofisi ya katibu wa 
UVCCM mkoa wa Shinyanga bi Regina Shija

Sinzo Khamis Mgeja akirudisha fomu ya kugombea ubunge 

wa viti maalum kundi la vijana mkoa wa Shinyanga

Sinzo Khamis Mgeja akisaini kitabu baada ya kurudisha fomu

Sinzo Khamis Mgeja akiwa na mdogo wake Mariam Khamis 

Mgeja ndani ya ofisi ya CCM mkoa wa Shinyanga
Sinzo Khamis Mgeja akiwa na mke wa mwenyekiti wa CCM 
mkoa wa Shinyanga /mama Mgeja(katikati) na Mariam Khamis 
Mgeja (kushoto) waliomsindikiza wakati wa kuchukua fomu ya
kuwania ubunge wa viti Maalum kundi la vijana mkoa wa Shinyanga


Sinzo Khamis Mgeja akiwa na mke wa mwenyekiti wa CCM 

mkoa wa Shinyanga /mama Mgeja(katikati) na Mariam Khamis
Mgeja (kushoto) .

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI