
Kwa mujibu wa Kaka wa Marehemu,Jabir
Ally Masanja,alisema Banza Stone,alifariki majira ya saa saba mchana,kutokana na kukabiliwa na maradhi ya Saratani ya Kichwa.
Alisema kutokana na maradhi hayo hivi karibuni alilazwa katika hospitali ya Mwananyamala,ambapo baada ya matibabu na hali yake kutia matumaini,alirejea nyumbani hadi mauti yalipomfika.
Jabir alisema maziko yatafanyika katika Makaburi ya Sinza Vatican kesho majira ya saa Kumi.