Friday, July 17, 2015

ACT WAZALENDO KUTOA MGOMBEA URAIS BAADA YA AGOSTI 13.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



CHAMA cha ACT Wazalendo,baada ya Agosti 13 kinatarajia kumpata Mgombea wake atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika

kinyang'anyiro chaUrais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25,mwaka huu.
 

Katika taarifa ya chama hicho iliyotolewa kwa waandishi wa habari jana na Naibu Katibu Mkuu,ACT Wazalendo Msafiri Mtemelwa, alisema tarehe hiyo ndipo Halmashauri kuu itakapokutana,kwa ajili ya kuteua jina la mgombea Urais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na kupendekeza majina ya wagombea Urais kwenye mkutano mkuu.

Alisema baada ya Kikao hicho cha Halmashauri Kuu ndipo kitafuatiwa na Mkutano mkuu utakaomchagua mtu atakayepeperusha bendera ya Chama hicho katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
 

Naibu Katibu mkuu huyo aliendelea kusema kuwa kuanzia Julai mosi mwaka huu Chama kilifungua rasmi pazia la uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi  za uongozi, kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi katika Nafasi za Udiwani na Ubunge.

Alifafanua kuwa tangu kuanza kwa uchukuaji huo wa fomu kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanachama wa chama hicho kuchukua fomu hizo kutokana na baadhi ya majimbo na kata kuwa na watia azma kuanzia wanne mpaka tisa,na kudai kutokana na hamasa hiyo ya wanachama wanahakika ya kusimamisha wagombea katika  majimbo 265 yakiwamo majimbo mapya 26 yaliyoongezwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).


Alisema kwa kipindi hiki kifupi tayari wameshakuwa na waweka azma zaidi ya mmoja katika majimbo 226 kwa nchi nzima,huku wakiwa na imani mpaka kufikia mwisho wa uchukuaji fomu ndani ya Chama majimbo yote 265 yatakuwa yanawatia azma mbali mbali wanaosubiri kupitishwa na chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu.


Katika Taarifa hiyo ilieleza kuwa kutokana mwitikio huo ni faraja kubwa kwa chama hicho amabcho bado kichanga,huku akidai kuwa mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi ya udiwani ni julai 24, kwa nafasi ya Ubunge mwisho julai 31 na nafasi ya Urais mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Agosti mosi.

Hata hivyo Taarifa hiyo ilibainisha kuwa tarehe hizo pia zianaweza kusogezwa mbele kwa sababu maalum na uamuzi unaweza kufanywa na Sekretariti ya Chama baada ya kukaimu baadhi ya majukumu ya kamati kuu,na kusisitiza kuwa Mwisho wa uchukuaji na urudishaji wa fomu hizo utafuatiwa na vikao mbali mbali vya uteuzi kwa ngazi husika kabla ya kufika katika ngazi ya Taifa.

Aidha alisema pamoja na mafanikio ya muda mfupi iliyopata ACT-Wazalendo lakini kumejitokeza baadhi ya watu  wanaokifanyia  michezo michafu kwa kuwarubuni na kuwahadaa waliotia azma ya kugombea nafasi mbali mbali hususani katika  maeneo ambayo kuna uduni wa mawasiliano.


Akifafanua alidai kuna taarifa walizozipata hivi karibuni  kutoka katika miji ya Tarime na Rorya Mkoani Mara kuwepo kwa baadhi ya watu wanaopita na kutangaza kuwa ACT Wazalendo,kimezuiwa kushiriki Uchaguzi kwa muda wa miezi sita,jambo ambalo si kweli na kuomba wananchi wapuuze taarifa hizo.
 

Ilisema taarifa hiyo kuwa chama kimebaini lengo la upotoshaji huo ni kukidhoofisha kutokana na ukuaji wake wa kasi kwa kuwakatisha tamaa Watanzania ambao wameanza kukiamini kutokana na dhamira yake nzuri ya kuirudisha nchi katika misingi iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius Nyerere.


Taarifa hiyo iliwahakikishia  wananchi kuwa Chama chetu kitashiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu kwa kuweka wagombea wa nafasi zote na Chama hakitakuwa tayari kuona sehemu yoyote ya nchi mgombea wa CCM anapita bila kupingwa.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI