Dr.Gerald Mwanzia akionyesha Fomu alizochukua za Udiwani. |
Kada
huyo wa CCM,mwenye taaluma ya Daktari wa binadamu,Dk.Gerald Mwanzia,alichukua
fomu hiyo na kukamilisha idadi hiyo ya makada watano,huku akisema iwapo atapata
ridhaa ya kuongoza Kata hiyo atahakikisha anaboresha sekta zote zilizozorota
kipindi akiwa hayupo madarakani.
Dk.Mwanzia
alisema kuwa kipindi akiongoza Kata hiyo,alifanikisha kukamilisha ujenzi wa
maabara ya sayansi katika Shule ya Sekondari ya Kata hiyo,kabla hata ya agizo
la Rais wa Jamhuri ya Muungano alilotoa kuwepo kwa maabara hizo kwa kila
sekondari za serikali nchini.
MTANGAZAJI wa Baloha FM,Ndalike Sonda,akifanya mahojiano na Dr.Mwanzia. |
Mbali
na Dk,Mwanzia ambaye alichukua fomu na kuirejesha,wengine waliochukua na
kurejesha ni pamoja na mwanajeshi mstaafu wa JWTZ,Pili Izengo,Mwanamichezo
maarufu katika Kata hiyo,Pazi Majuto
Pazi,aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Bandari,Said Hamadi “Shantuti”na
Justine Akuziwe.