MGOMBEA
nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha
Mapinduzi “CCM” Dr.John Pombe Mgufuli, ameendeleza kauli yake ya kudai
hatowaangusha Watanzania pindi
akichaguliwa katika wadhifa huo Oktoba
25,mwaka huu huku akidai wakati utakapofika atakuwa na ahadi yenye neema
kwa wakazi wa wilaya ya Kahama.Akizungumuza na wanachama wa Chama cha Mapinduzi,waliojitokeza katika ofisi za chama hicho wilaya ya Kahama,Dr.Magufuli alisema amepita kujitambulisha kwa wakazi wa wilaya ya Kahama akitokea mkoani Geita,hata hivyo alisema changamoto za wilaya ya Kahama anazifahamu wakati utapofika atazianisha fursa za kuzitatua.
Alisema
anatambua ukubwa wa mji wa Kahama na kasi ya maendeleo iliyopo
halingani na hadhi iliyonayo, na kuwahakikishia kuwa kulingana na ilani
ya chama chake wilaya hiyo itafikia hadhi stahili kulinagana na ukuaji
wake.
Alisema kuwa mji wa Kahama ambao umepewa hadhi ya Manispaa
hivi karibuni,unastahili kupata hadhi inayolingana na ukuaji wake hatua
itakayosaidia ukuaji wa kasi wa maendeleo.
Alisema kuwa ipo mikoa mingi hapa nchini ilipewa hadhi ya kuwa mkoa lakini haijafikia idadi ya watu waliopo wilayani Kahama,jambo analofikiria atakapofika katika Kampeni atahakikisha anasimamia ilani ili wilaya ya Kahama ipate stahiki yake kulingana na kasi ya maendeleo yake.
Alisema kuwa ipo mikoa mingi hapa nchini ilipewa hadhi ya kuwa mkoa lakini haijafikia idadi ya watu waliopo wilayani Kahama,jambo analofikiria atakapofika katika Kampeni atahakikisha anasimamia ilani ili wilaya ya Kahama ipate stahiki yake kulingana na kasi ya maendeleo yake.
“Naomba muendelee
kuniombea kama nilivyowaomba wakati wa mchakato ndani ya chama,kwani
miundo mbinu ya wilaya yenu inahadhi ya juu kuliko mliyonayo,lakini
nadhani haitoshi,nitaelezea bulungutu lote la ilani imelenga kufanya
nini kwa Kahama wakati ukifika,wana Kahama sintowaangusha,”Alisema.
Aidha alisema katika utawala wake kila mwananchi atakuwa na haki kwa kila Nyanja ili kuendelea kudumisha umoja wa Kitaifa na kuondoa matabaka ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani kutokana na baadhi ya watu kujiona ni bora kuliko wengeine inayosababishwa na kuwepo kwa matabaka.
Alisema atahakikisha anadumisha msingi imara wa upendo pasipo kujali tofauti za kiitikadi za vyama,dini ama kabila hatua itakayosaidia kuondoa matabaka ya baadhi ya Watanzania kuona miongoni mwao ni bora kiasi cha kufikia kuogopwa na kutoshirikiana na wengine jambo ambalo ni kukiuka mila na desturi za Kitanzania.