Wednesday, June 24, 2015

SKAUTI YATOA MAFUNZO YA UKAKAMAVU KWA VIJANA 3500

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MGENI rasmi Sweetbert Nkuba.
KATIKA kuimarisha afya kwa vijana mashuleni na kuwaepusha na maradhi ya mara kwa mara,Chama cha Skauti Tanzania Mkoani Shinyanga kimetoa mafunzo ya ukakamavu kwa vijana 3500 katika
vikundi 50 vilivyoko katika shule mbalimbali za Msingi na Sekondari.
MWENYEKITI wa Baraza la Skauti Mkoa wa Shinyanga,Omari Mziya.
KIAPO cha Skauti.

Hali hiyo ilielezwa juzi mjini Kahama  na Kamishina  wa Skauti, Mkoa wa Shinyanga, Mussa Chama,wakati wa uzinduzi wa Baraza la Skauti Mkoani Shinyanga uliokwenda sambamba na kusimikwa kwa Mwenyekiti mpya wa baraza hilo.
SKAUTI kikaoni.

 Chama alisema Skauti mkoa mbali na kutoa mafunzo hayo ambayo yamelenga kuimarisha afya za vijana ili kuepukana na magonjwa nyemelezi ya mara kwa mara pia mafunzo hayo yamewawezesha kuwa na uwezo wa kujitegemea katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali ikiwemo kazi ndogondogo za kiuchumi.
MGENI rasmi Sweetbert Nkuba akiongea.

Katika uzinduzi huo,Chama alisema tayari kamati yake imezunguka mkoa mzima na kuunda vikundi hivyo hamsini vyenye wanachama 50 ambao tayari wamepatiwa mafunzo ya ukakamavu,na ujasiri wa kujitegemea pasipo kutegemea ajira ya kuajiriwa,hatua itakayosaidia kuinuka kiuchumi kwa vijana na taifa kwa ujumla.
MWENYEKITI wa Baraza la Skauti mkoa wa Shinyanga,Omary Mziya akiongea na Skauti.
 Hata hivyo alisema pamoja na mafunzo hayo vijana wengi wamekuwa na changamoto kubwa ya kutoelewa mafanikio ya skauti hali ambayo wakati mwingine imekuwa ikileta vikwanzo wakati wa utoaji mafunzo hayo.
WAJUMBE wa Baraza la Skauti mkoa wa Shinyanga.

 Nae mlezi wa skauti Wilaya ya Kahama katika Halmashauri ya Mji ALuko Lukolela alisema ili kuimalisha vijana hao licha ya kuwapa mafunzo ya ukakamavu lazima wawe na vikundi vya uzalishaji mali.
 Lukolela ambaye pia ni Afisa Elimu wa Mji wa Kahama alisema vijana hao bado wanafurusa kubwa ya kujiimalisha kiuchumi kwa kuwa na miradi ya uzalishaji kuliko kuwa na ukakamavu wakati wakiwa na changamoto za kiuchumi.
MWENYEKITI wa baraza la Skauti,Mziya akisisitiza jambo.
Aliwataka kuhakikisha wanaibua miradi mingi katika sekta za kilimo na ufugaji ambao utawasaidia kuimarisha maisha yao ama kusaidika kwa njia rahisi zaidi.

 Kwa upande wake mwenyekiti mpya wa baraza la skauti Mkoa wa Shinyanga  Omary Mziya aliahidi katika kipindi chake cha miaka mitatu ya uongozi wake atahakikisha anawaandaa vijana katika maisha ya kujitegemea.
MLEZI wa Skauti wilaya ya Kahama,Aluko Lukolela aliyeipa mgongo kamera,akiwapongeza wajumbe wa baraza la Skauti Mkoa wa Shinyanga,mara baada ya kuapishwa kwao.


Mziya alisema vijana hao kama wataandaliwa kwenye shughuli za kiuchumi yapo mafanikio makubwa ya kiuchumi
 kwa Taifa lijalo kuliko kuwafundisha ukakamavu na kisha kuwaacha wakizagaa mitaani.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI