BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO
 |
AFISA Matekelezo na Uratibu kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya {NHIF},Makao Mkuu Dar Es Salaam;Catherine Masingisa,akiwasilisha mada kwa wajumbe. |
WATUMISHI wa Idara ya Afya katika Hospitali
ya Wilaya ya Kahama ambao wamekuwa
wakiiba dawa zinazotolewa
na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)wameonywa
kuondokana na tabia hiyo kutokana na kuwaumiza Wananchi walio wengi wa hali ya
chini wanaokwenda kupata matibabu Hospitalini hapo.
 |
MGANGA Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Dkt.Bruno Minja,akitoa ufafanuzi kwa wajumbe. |
Hayo yalielezwa juzi na Mkuu wa Wilaya ya
Kahama,Benson Mpesya,wakati akifungua mafunzo kwa ajili ya uendeshaji wa Mfuko
wa Afya ya jamii Mjini uliojumuisha Watendaji wa Halmashauri ya Mji, Wadau
mbalimbali wa Afya, Madiwani pamoja na watu mashuhuri na kuonya juu ya tabia
hiyo kuwa inamkandamiza Mwananchi wa hali ya chini.
 |
AFISA Mtendaji wa Kijiji cha Nyihogo,Mabumba,akiuliza swali. |
Alisema kuwa Baadhi ya watumishi wa Idara ya
Afya pamoja na kuwa na mishahara mikubwa ya hali ya juu wamekuwa ndio chanzo
kikubwa cha kuiba dawa zinazotolewa na Bima ya Afya na kuhamishia katika maduka
yao yaliopo nje ya Hospitali ya Wilaya.
 |
MKURUGENZI wa Mfuko wa Afya ya Taifa ya Jamii Tanzania {CHF},Eugen Mikongoti,akijibu moja ya maswali ya wadau. |
“Nashangaa huwezi kugeuka kutoka katika fani
ya udaktari hadi kuwa mwizi wa dawa hali hii ni aibu, Mwananchi anatoka
kijijini kuja kupata matibabu Hospitalini anaambiwa hakuna dawa na aende
kununua katika maduka yaliopo nje ya Hospitali ambayo yanamilikiwa kwa kiwango
kikubwa na Madaktari hao ni aibu”, Alisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama.
 |
MIONGONI mwa Wadau waliohudhuria warsha hiyo ya siku Moja. |
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) Michael Mhando
alisema kuwa Mfuko huo wa Afya jamii Mjini utasimamia matibabu kwa mfumo wa tiba
kwa kadi (TIKA) utasaidia katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa
mikopo ya vifaa mbalimbali vya Afya katika vituo mbalimbali vya Afya bila ya kujali ni vya binafsi au vya Serikali.
 |
DIWANI wa Viti Maalumu wa Halmashauri ya Mji kupitia tiketi ya CHADEMA,Winfrida Daud,akichangia mada. |
Alisema kuwa pia mfuko huo utapata nafasi ya
kutoa ushauri mbalimbali wa kitaalamu
katika Halmshauri husika na kuongeza kuwa mfuko huo katika Halmashauri ya mji
wa Kahama umekuwa ukisuasua kutokana na hali hafifu ya uchangiaji hali ambayo
imefanya kuwa kati ya kaya 49,437 zilizopo katika Halmashauri hiyo ni kata 715
tuu ambazo tayari zimechangia katika kupata huduma hiyo.
 |
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Machibya Kiduramabambasi,akiongea na wajumbe. |
Aliendelea kusema kuwa ili kudumisha mfuko
huo wa Afya ya jamii Mjini Mfuko wa Bima ya Afya umependekeza asilimia 67 ya
michango itakayochangwa katika mfuko huo itapelekwa katika manunuzi ya dawa
kuondokana na malalamiko mengi yalikokuwepo katika mfuko wa CHF uliokuwa
ukitumika hapo awali.
 |
MKUU wa wilaya ya Kahama,Benson Mpesya,akifungua Warsha hiyo. |
“Kwa sasa CHF itajihusisha katika Halmashauri
za Wilaya tuu lakini Mfuko wa Afya ya jamii mijini (TIKA) yaani Tiba kwa kadi itajihusisha
katika Halmashauri za Miji, Manispaa pamoja na Majiji hali ambayo kwa hivi sasa
ndio wanaitungia sheria ndogo ili iweze kutumika kwa Wananchi”, Alisema Michael Mhando.
 |
KAIMU Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Taifa Nchini,Michael Mhando,akitoa ufafanuzi wa majibu juu ya maswali yaliyoulizwa na wajumbe. |
 |
MJUMBE kutoka Kanisa la KKKT mjini Kahama,Imelda Theonest,akiuliza swali. |
Alisema kuwa Sheria hiyo itaangalia katika
kuweka Viwango vya uchangiaji, Viwango vya watu ambao watakuwa hawana kadi za
kutumia katika matibabu,Viwango vya adhabu pamoja na wajibu wa utoaji wa huduma
hiyo na pia kuangalia ni nani atakuwa na dhamana hiyo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI