BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO
 |
Rais Jakaya Kikwete akiweka mchanga katika kaburi la Mufti Simba katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga | |
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete,amewaongoza maelfu ya waumini wa Dini ya kiislamu na watu
wengine wenye imani mbalimbali,kumzika Sheikh Mkuu wa
Tanzania,Mufti
Alhaji Sheikh Shaaban bin Simba
katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga.
 |
WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya tatu,Fedrick Sumaye |
Maziko hayo yalifanyika jana baada ya mshuko wa sala ya Alaasiri na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu,wakristo na viongozi wa serikali ambao
walijitokeza kumzika Mufti Simba aliyefariki dunia juzi akipatiwa matibabu kutokana
na kusumbuliwa sana na sukari,Shinikizo la Damu (BP) pamoja na Figo.
 |
WAZIRI Mkuu aliyejiuzuru katika Serikali ya Awamu ya Nne,Edward Lowassa. |
Mwili wa marehemu uliwasili mchana mjini Shinyanga ukitokea
jijini Dar es salaam na kufikishwa nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Majengo
kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga.
 |
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Tanzania,Benard Membe. |
Baadaye mwili ulipelekwa katika msikiti wa Masjidu Thaqafal Abdallah Islamiya uliopo
Majengo mjini Shinyanga kwa ajili ya sala ya alasiri kisha mwili huo kupelekwa
katika makaburi ya Nguzo Nane kwa ajili ya Maziko.
 |
Kadhi mkuu wa Tanzania Sheikh Yusuph Bin Abdalla Mnyasi akiweka mchanga kwenye kaburi. |
Pia watia nia mbalimbali wa nafasi za Uwakilishi katika majimbo ya mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na Watia nia wanne wa urais Lazaro Nyalandu,Fredrick
Sumaye,Edward Lowassa na Bernard Membe pia wamelihudhuria maziko hayo.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI