Hayo yalibainishwa juzi na Mwenyekiti wa Buika SACCOS, Agapiti Kisoka, katika hafla fupi ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 900 kutoka katika Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa lengo la kukuza mtaji kwa Chama cha kuweka na kukopa kilichopo mgodini hapo.
WANACHAMA wa Buika SACCOSS |
Kisoka alisema asilimia kubwa ya wafanyakazi walio wengi walikuwa wakifanya kazi huku wakienda kuangalia mafao yao kila mwezi katika mifuko hiyo ya pensheni hali ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa wafanyakazi katika migodi hiyo pindi wanapoona wanakiasi kikubwa cha fedha walichochangia katika mifuko hiyo.
MENEJA wa PPF tawi la Kahama,James. |
Alisema kutokana na hali ya mfuko huo wa PPF kwa kutoa fedha hiyo ili kuzidi kuiongezea mtaji Saccos ya Buika ambayo mpaka kufikia sasa ina wanachama 634 sawa na asilimia 30 ya watumishi wa mgodi huo,utasaidia kuendelea kuwapa nafuu ya maisha wanachama wake.
“Fedha hizi zilizotolewa na mfuko wa pensheni wa PPF zitatusaidia katika mambo mbalimbali yakiwamo ada za watoto pamoja na matatizo mbalimbali ya kijamii yanayotokea katika familia za wafanyakazi kwa mikopo ya papo kwa papo kwa kiwango kisichozidi milioni moja,”alisema mwenyekiti huo.
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini,Charles Kitwanga na Meneja wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Michelle Ash,wakifurahia jambo. |
Alisema mkopo uliotolewa kwa wafanyakazi hao utakuwa na kiwango cha riba nafuu ya asilimia kumi na itatolewa kwa kipindi cha kuanzia miaka tatu hadi mitano na kuongeza kuwa sharti la kupata mkpo huo nikuwa mwanachama wa PPF.
MENEJA Ufanisi wa Kampuni ya dhahabu ya Bulyanhulu inayomilkiwa na ACACIA,Elias Kasitila anayeandika akiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa PPF,Selestine Some. |
NAIBU Waziri Charles Kitwanga,akihotubia. |
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga alimuomba Meneja
wa Mgodi huo Michelle Ash kuangalia uwezekano wa kuwaongeza fedha kwenye mfuko
huo ili wafanyakazi wapate hamasa na kumudu kukopa kiasi kikubwa cha pesa ili
kukidhi mahitaji yao.