Thursday, July 2, 2015

VIONGOZI WATAKIWA MAHUSIANO MAZURI NA JAMII ZINAZOZUNGUKA MIGODI.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

 WITO umetolewa kwa Viongozi wa Serikali ngazi ya kata  kujenga mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka katika maeneo yanayozunguka Migodi ya Acacia Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ili kuepusha
migogoro ya ardhi inayoweza kutokea na kusababisha uvunjifu wa amani.


 Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Elikana Masota katika  Mafunzo ya Amani endelevu na ulinzi na usalama katika maeneo yanayozunguka migodi ya Acacia yaliondaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Search For Common Ground La Mjini Kahama.


 Katika mafunzo hayo yaliojumuisha yaliojumuisha viongozi mbalimbali kutoka katika kata zilizo jirani na Migodi ya Dhahabu ya Bulyanhulu pamoja na Buzwagi yallikuwa na lengo  la kuelimisha viongozi hao juu ya Sera ya ardhi ili kutokuleta mifarakano na wawekezaji.


 Alisema kuwa migogoro mbalimbali inayotokea imekuwa ikisababishwa na kutoshirikishwa kwa Wananchi katika kutatua matatizo mbalimbali yanayohusika na ardhi hali ambayo inasababisha mifakano baina ya  Mwekezaji na mmiliki wa ardhi wakati  malipo ya fidia

Alisema kuwa kwa sasa Wananchi lazima watambue Sheria na kanuni mbalimbali zinazohusu masuala ya ardhi hali ambayo kwa kutumia viongozi hao walipata mafunzo wataweza kuifikisha katika jamii husika kwa kutumia vikao  mbalimbali au mikutano ya hadhara.


Aidha alisema kuwa ushirikiano katika kutatua migogoro ya ardhi ni suala la msingi na kuiongeza kuwa kufanya hivyo migogoro inaweza kutatuliwa huko huko katika eneo husika kabla ya kufikishwa  Mahakama za ngazi ya juu.
Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Search for Common Ground Lazaro Mapimo alisema kuwa  Shirika lake linafanya kazi katika nchi 34 Duniani na kuongeza kuwa katika ya Tanzania shirika hilo linafanya kazi Wilayani Katika Mioigodi ya Acacia Bulyanhulu pamoja na Buzwagi, Mkoani  Mara katikam Mgodi wa Norh Mara pamoja na Visiwani Zanzibar.
Alisema kuwa kwa muda wa miaka mitano tangu shirika hilo lianze kufanya kazi hapa nchini limeweza kutoa mafunzo mbalimbali ya juu ya ujirani Mwema baina ya Wananchi wanazunguka Migodi na tayari mafanikio yamekwishaanza kuonekana katika maeneo mbalimbali kwani  Wananchi wameanza kujua stahiki zao.





KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI