Thursday, June 11, 2015

KINGWANGALLA;HAKUNA MZOEFU KWENYE MADARAKA YA RAIS.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO

MBUNGE wa jimbo la Nzega,Hamis Kigwangalla,akiongea na umati wa watu kutoka Mikoa ya Tabora na Shinyanga katika Viwanja vya Packing mjini Nzega,waliofika kumsikiliza wakati akitia nia ya kuwania nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


MBUNGE wa jimbo la Nzega mkoani Tabora  Dkt,Hamisi  Kigwangalla
amesema kuwa hakuna uzoefu katika nafasi ya Urais bali wenye uzoefu

huo wapo wanne ambao tayari wamekwisha pitia nafasi hiyo na kukaa
kwenye  jengo la Ikulu  ambao aliwataja kuwa Baba wa Taifa Mwl,Julius
Nyerere,Ali Hassani Mwinyi,Benjamini Mkapa  na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.


VIJANA walikuwa watulivu kumsikiliza Kigwangalla.

Akihutubia wananchi wa Jimbo la Nzega wakati wakutangaza nia ya
kuwania nafasi kubwa ya kuteuliwa kuwa mgombea Urais  kupitia  chama
cha mapinduzi CCM  katika viwanja vya parking mjini Nzega
Dkt,Kigwangalla  alisema wengine wote waliobaki sio wazoefu wa kufanya
kazi Ikulu bali ni wazoefu wa shughuli nyingine.

MBUNGE wa Jimbo la Nzega Hamis Kigwangalla akieleza vipaumbele vyake
Alisema kuwa wote wanao wania nafasi hiyo akiwepo yeye mwenyewe
wanauzoefu tofauti tofauti katika masuala mbalimbali huku akiwabeza
wenye uzoefu wa ubadhilifu wa mali za umma ikiwemo Rushwa na ufisadi
hali ambayo akiteuliwa na kushinda nafasi hiyo atapambana na vyo.
SEHEMU ya umati waliohudhuria kumsikiliza Mtia nia Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Hamis Kigwangalla,katika viwanja ya Packing mjini Nzega.
“……wapo wazoefu ambao wamekaa Ikulu nakulitumikia taifa hili kwa
vipindi tofauti tofauti lakini sio hao leo hii wanaomba nafasi ya
kuteuliwa na chama kwa ajili ya kuwa rais wanchi hii kwani wote tuko
sawa kwa kuwa hakuna aliye wahi kufanya kazi Ikulu kama Rais wa
Nchi’’alisema Kigwangalla.

MBUNGE wa Jimbo la Nzega,Hamis Kigwangalla akiongea juu ya nia yake ya kuwania Urais wa awamu ya tano .


Kauli hiyo ilikuja baada ya kuwepo madai ya kuwa vijana wenye umri
mdogo hawa wezi kuongoza Nchi kwa tabia iliyojengeka katika yakuwa
watu wenye umri mkubwa unao zidi  miaka 40 ndio wenye uwezo wa kuwa
ongoza watanzania hali ambayo alipingana nayo kwa madai hata wenye
umri mkubwa wapo ambao hawana uwezo wa kuongoza.

MH;Kigwangalla kwa umakini mkubwa akieleza vipaumbele vyake.

Dkt,Kigwangalla katika vipaumbele vyake iwapo atateuliwa na kushinda
nafasi hiyo atahakikisha ndani ya mwaka mmoja watanzania wote watakuwa
na Bima ya Afya watakao lipiwa na Serikali pamoja na kuwa jari
watumishi wa Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili waweze kutoa huduma
bora ya matibabu kwa wananchi.

UMATI ulimsikiliza kwa makini.

“…….iwapo watanzania hawata pata huduma bora ya Afya kama kiongozi wa
Nchi mwisho wa siku utaongoza Taifa la wagonjwa na hivyo kudhoofisha
nguvu kazi ya Taifa hali ambayo inayoweza kusababisha kushuka kwa
uchumi wa Nchi’’alisema dkt Kigwangalla.



Alisema katika kuboresha suala la Elimu kwa watanzania kama atashika
nafasi hiyo anatamanai Elimu yote kuanzia Awari,msingi na sekondari
bure kwa kuwa atahakikisha nchi inakuwa na uchumi imara kwa kupunguza
matumizi ya serikali,safari,posho na ukubwa serikali.


MH:Kigwangalla akimwaga sera.

Akizungumzia suala la kukuza uchumi kwa wakulima,wafanya Biashara
wadogowadogo na viwanda anatamani kuanzisha mfuko wa kukopesha
wananchi kwa kuwekeza Bill 500 kwa mwaka pamoja na kuboresha kitengo
cha ustawi wa jamii katika Halmashauri kwa ajili ya kwa
Elimisha,kuwaunganisha kwenye vikundi vya kudhaminiana na kuratibu
shughugili zao.

VIWANJA vya Packing vilifurika umati uliofika kumsikiliza Mh;Kigwangalla.
MBUNGE Kigwangalla akitaja vipaumbele vyake.
Hata hivyo alisema anatangaza rasimi kuwa ana nia ya dhati ya
kuwapeleka watanzania kwenye nchi ya ndoto na ahadi zawaasisi wetu na
kwamba kama atateuliwa na chama chake kugombea urais wa Jumuhuri ya
Muungano wa Tanzania mwaka 2015 atahakikisha mambo matatu muhimu
anayafanyia kazi, ambayo kuondoa umasikini na kukuza uchumi kwa
malengo ya kuzalisha fursa nyingi zaidi za ajira nchini.
Alisema kwa kufanya hivyo Serikali itakuwa inauwezo wa kuzalisha ajira
rasimi laki mbili kila mwaka na ajira zisizo rasimi milioni kumi kila
mwaka na uchumi huu utamgusa kila mtu kila mwaka.


Kipaumbele kingine alisema ni kutoa huduma bora za
kijamii,Afya,Maji,Elimu,
miundombinu ya Barabara na Umeme pamoja na
kudumisha utawala bora.

WAKIFUATILIA hotuba ya Mbunge Kigwangalla.
MBUNGE wa Jimbo la Nzega,Hamis Kigwangalla,akiingia uwanja wa Packing Mjini Nzega,kueleza nia yake ya kujitosa kuwania nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
Pia alisema atahakikisha anapambana kwa nguvu zote kuhakikisha anakomesha mauaji ya watu wenye Ulemavu wa Ngozi "Albino"kwa kuhakikisha kesi hizo hazichukui muda mrefu,sambamba na Mahakama zake kuzifanya wazi ili kila Mtanzania mwenye lengo la kufuatilia mashauri hayo apate fursa hiyo.
MBUNGE Jimbo la Nzega,Hamis Kigwangalla akiongea na umati uliojitokeza kumsikiliza akitangaza nia ya kugombea Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM.
MH:Kigwangalla alipokuwa akiingia viwanja vya Packing.
MAKUNDI mbalimbali yalijitokeza kumuunga Mkono Mbunge wa Jimbo la Nzega,Hamis Kigwangalla,katika nia yake ya kujitosa katika kinyang'anyiro ndani ya CCM,kuwania nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI