na kujiwekea malengo ya kujikomboa kiuchumi na kijamii ili kupunguza vitendo vya manyanyaso ikiwemo ukatili wa Kijinsia.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti
wa Baraza la Wanawake la CHADEMA"BAWACHA",wilaya ya Msalala,Asha
Binde, wakati alipojumuika na wanachama Baraza hilo,kutembelea wagonjwa
waliolazwa katika Kituo cha Afya cha Lunguya kilicho Halmashauri ya Msalala
wilayani Kahama,ambapo alisema kujikomboa kiuchumi kutawaondoa katika vitendo vya kunyanyaswa.
Binde alisema wanawake waondokane na
dhana kuweza pasipo kuwezeshwa kila inapofika maadhimisho bali uwezesho huo uwe
endelevu katika maisha ya kila siku,kwa kujituma katika shughuli mbalimbali za
kijamii ili kuondokana na utegemezi,na nafsi zao zikitawaliwa na upendo,huruma
kwa jamii zenye matatizo.
“Dhana ya wanawake kuweza bila
kuwezeshwa iwe endelevu katika maisha yetu isingoje maadhimisho tu,tujitume
katika kazi na tuwe na huruma na upendo kwa jamii inayoguswa na matatizo kila
mara kwa kuwatembelea waagonjwa na kuwasaidia huduma mbalimbali mbali ya kuwapa
pole,”Alisema Binde.
Aidha
aliwaomba wanawake wajitokeze
kujiandikisha katika daftari la kudumu la upigaji kura sambamba na
kujitokeza
kuwania nafasi za Udiwani na Ubunge katika Uchaguzi mkuu wa mwaka
huu,ili kutumia fursa hiyo kama njia ya kupata haki zao zinazostahili.
Mwenyekiti huo wa Bawacha wilaya ya
Msalala aliwaomba wanawake wafanye mabadiriko ya kifikra kwa kuondokana na
mazoea ya kuchagua wawakilishi kwa kununuliwa bali yawe matakwa yao halisi kwa
kiongozi wanayemhitaji.