BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO
 |
WANACHUO Dastan Dickson aliyesimama na Benjamin Paul. |
VIJANA walioachishwa ajira
migodini kutokana kuwa na umri mdogo kisha kupelekwa chuoni kupata elimu ya
ufundi mbalimbali,wamedai elimu ya nadharia wanayopatiwa inawachanganya
hivyo
ni vyema wakapatiwa ya vitendo itakayokidhi malengo stahiki ya kupata ujuzi,utakaokuwa
mkombozi wa maisha yao.
 |
MKURUGENZI wa HUHESO Foundation,Juma Mwesigwa,kulia. |
Wakiongea mbele ya Uongozi
wa Shirika la The Foundation for Human Health Society HUHESO FOUNDATION,ambao
wanatekeleza kwa kushirikiana na mashirika matatu,kuwaondoa watoto
wanaotumikishwa kazi ngumu katika migodi midogomidogo iliyo wilayani
Kahama,vijana hao walidai kukabiliwa na changamoto nyingi chuoni hapo.
 |
MKUU wa Chuo cha Wananchi Malampaka,Sospeter Kugasa. |
Vijana hao 180,walisema
tangu wamefika chuo cha VETA, cha Wananchi Malampaka,wamekuwa wakipatiwa
mafunzo ya darasani huku wengi wao wakiwa hawajui kusoma na kuandika kutokana
na kutowahi kupelekwa shuleni,hivyo kuona wanapoteza muda wao iwapo
hawatapatiwa mafunzo kwa vitendo.
 |
WANACHUO wa Taaluma ya Ufundi gari. |
“Inashangaza kozi
tulizoahidiwa hazipo,na kibaya Zaidi kwa wanaochukua ufundi wa kutengeneza
magari wanawekwa darasani,ama kuonyeshwa vipuri kupitia magari mabovu
yasiyotengenezeka yaliyopo chuoni,hawapati ujuzi ama uzoefu wowote ni vyema
wangetafutiwa gereji ili kupata ufundi kwa vitendo,hali ni hiyo hiyo kwa
wanaochukua ufundi wa umeme wa majumbani na viwandani”Alisema Richard Alex.
 |
WANACHUO katika kikao na Uongozi wa HUHESO Foundation. |
Aidha kwa wanaochukua
ufundi wa kushona nguo,walilalamika uchache wa vyerehani uliopo chuoni
usiolingana na idadi ya wanafunzi,sambamba nakutumia muda mwingi kutumikishwa
shughuli nyingine za kijamii chuoni hapo badala kupatiwa mafunzo ya ufundi huo.
 |
MWANAHABARI mtoto Irene akiwa katika mahojiano na wanachuo. |
 |
MWANACHUO Levania Adraham akitoa dukuduku lake. |
Vijana hao pia walilalamikia
suala la kupata maji safi na salama ambalo limekuwa ni tatizo kubwa kwao kiasi
cha kuathiri afya zao.
Mkurugenzi wa Huheso
Foundation,Juma Mwesigwa,aliwaomba vijana hao kuwa wavumilivu na kuwa
changamoto zinazowakabili watazishughulikia kwa ushirikiano wa mashirika
mwenza,mfadhili wa mradi Terre des Hommes pamoja na uongozi wa Chuo hicho.
 |
WANACHUO katika mahojiano na Wana Habari Watoto. |
Mwesigwa alisema ni budi
wazingatie nidhamu kwa kuwa ndio msingi wa maendeleo yao,kwa kutoipoteza fursa hiyo
waliyoipata kwaajili ya ukombozi wa maisha yao,na kuzingatia kwa bidii kile
wanachofundishwa katika fani wanazosoma.
 |
WANACHUO katika Kikao. |
Kwa upande wake Mkuu wa
Chuo Cha Wananchi Malampaka,Sospeter Kugasa,alikiri vijana hao wengi kuwa
hawajui kusoma na kuandika,lakini wamewafundisha na baadhi yao wameanza kupata
uelewa huo ambao ni msingi mkuu katika maisha.
 |
MWANAHABARI mtoto Irene katika mahojiano. |
Kugasa alisema pia
walipata changamoto kubwa ya kuwaweka sawa kisaikolojia kwa vijana hao ambao
walikuwa tayari walikuwa wameishazoea kupata pesa,huku wakifika chuoni na hofu kwa
kudhani maisha ya shule ni ya kupewa adhabu,na kuwatoa hofu vijana hao kuwa
watapatiwa mafunzo yanayostahiki.
 |
MWALIMU Dotto Felician,akifundisha kwa vitendo namna ya kuchomelea vyuma. |
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI