Sunday, January 25, 2015

PROFESA MUHONGO AJIUZULU.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO


HATIMAYE   Profesa Sospeter Muhongo amemwandikia Rais Jakaya Kikwete barua ya kujizulu rasmi wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania, kufuatia
sakata la Tegeta Escrow lililotikisa nchi kwa muda mrefu.

Akiongea na Waandishi wa Habari,Profesa  Muhongo,alidai mtu safi na hajahusika katika kadhia hiyo ya rushwa ya uchotwaji wa mabilioni ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Hata hivyo alisema ameamua kujiuzulu bila kupata shinikizo akiona kwamba yeye ndio atakayemaliza mjadala huo wa sakata ya rushwa ya Tegeta Escrow.

Ameahidi kuzungumza na watanzania hivi karibuni ili kuwaeleza undani wa  ukweli wa akaunti ya Tegeta Escrow.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI