MCHUNGAJI msaidizi Moses Daud aliyechuchumaa akijenga ukuta wa choo. |
KANISA la Healing
&Refugees Tanzania Church “HRTC” lililo Kata ya Nyihogo Mjini Kahama wilaya
ya Kahama mkoani Shinyanga limelifungwa na
Halmasahuri ya mji wa Kahama baada
ya kubainika halina vyoo vya kujisaidia waumini wake.
ya kubainika halina vyoo vya kujisaidia waumini wake.
Kwa mujibu wa barua
iliyoandikwa na Kaimu Mkuu wa Idara wa Usafi na Mazingira katika Halmashauri
hiyo ya Mji wa Kahama,Johannes Mwebesa,ilionesha Kanisa hilo alilifunga Desemba
29 mwaka jana,ingawa kufungwa rasmi lilifungwa na Polisi Januari 8,mwaka huu.
WAKISHIRIKI kujenga choo |
Katika barua hiyo
iliyosainiwa na Mwebesa na nakala kupelekwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Mji wa Kahama,ilieleza kulifunga Kanisa hilo baada ya kubaini kufanya ibada
zake bila kuwa na vyoo ambapo ni kinyume na sheria ya mazingira isiyoruhusu
kukusanya watu bila kuwa na sehemu ya kujisaidia.
Hata hivyo uamuzi huo
umepingwa na Wachungaji wa kanisa hilo;Moses Daud na Joshua Machibya ambao
walidai uamuzi huo haujawatendea haki kutokana na nguvu kubwa iliyotumika
kufunga Kanisa hilo kwa kutumia Polisi.
MCHUNGAJI Mkuu wa Kanisa la HRTC;Joshua Machibya akibeba tofari. |
Mchungaji Msaidizi wa kansa hilo, Daud,alisema yeye na waumini wake walishangazwa na kitendo cha Halmashauri hiyo,kuwavamia na kufunga kanisa lao bila maelekezo yoyote ya ujenzi stahili wa vyoo.
Alidai wanavyofahamu walipaswa kukaguliwa kisha kupewa maelekezo sambamba
na muda wa ujenzi wa vyoo,hasa kwakuwa tayari waumini walikuwa na choo kingine
cha muda walichokuwa wakitumia wakati taratibu za ujenzi zikiendelea, lakini walichofanya
ni kufunga kanisa.
MCHUNGAJI Mkuu;Joshua Machibya kulia akimkabidhi tofari Mchungaji Msaidizi;Moses Daud,ili kuendelea na ujenzi. |
Alisema pamoja na kufika
ofisini kwao kwa ajili ya kuomba muda hawakusikilizwa na badala yake Januari
8,mwaka huu walifikiwa na Polisi kwa vitisho mbalimbali kama wao kazi wanayo
ifanya kwa maslahi yao ambapo ni kwa maslahi ya kiroho.
WAKIENDELEA na Ujenzi wa Choo cha Wanawake. |
Naye Mchungaji Machibya ambaye
ndio Mchungaji Mkuu wa Kanisa hilo alisema kilichomshangaza yeye watumishi wa
Idar ya Mazingira kuja na Polisi kuwakamata wakidai wamekaidi amri ya kulifunga
Kanisa hilo,hali ambayo ilikuwa na vitisho vikubwa kinyume na taratibu za
kibinadamu.
Naye Mwebesa Kaimu Idara
ya Usafi na Mazingira katika Halmashauri hiyo,jana alipotakiwa kuzungumzia hali
hiyo alikiri kulifunga kanisa hilo kwa madai yupo kisheria kutokana na Kanisa
hilo kufanya shughuli zake bila kuwa na huduma ya vyoo kwa waumini wake.