NGONO YA MDOMO INASABABISHA SARATANI YA KOO JAMANI
SARATANI imeendelea kuwa
tishio hapa nchini huku hofu ikiendelea kuikumba jamii kutokana na
wataalamu wa afya kushindwa
kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo hatari.
kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo hatari.
Takwimu
kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha ongezeko la
saratani ya mdomo na koo kwa kiasi
kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006 hadi 277 mwaka 2012.
kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006 hadi 277 mwaka 2012.
Mkurugenzi wa Idara ya
Kinga Ocean road, Julius Mwaiselage anaeleza kuwa watanzania wasipende
kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya
mapenzi kwa njia ya mdomo. “Saratani ya mdomo ipo, na nyingine
zinasababishwa na zinaa “ anasema Dk Mwaiselage
Tafiti mbalimbali
zimewahi kufanyika nchini na kubaini kuwepo kwa ongezeko la saratani ya
mdomo.Utafiti uliofanywa na Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia
cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umebaini aina za saratani
1,594, kati ya hizo 509 zikiwa ni za midomo kwa mwaka 2003 pekee.
Matokeo hayo yanaonyesha
kuwa kati ya saratani 509 za mdomo, saratani 242 zilisababishwa na
Virusi vya Human Papiloma ambavyo hutokana na zinaa. “Ninachojua
mimi ni kuwa Virusi vya HPV husababishwa na magonjwa ya zinaa, hivyo
mtu anayeugua saratani ya aina hiyo, imetokana na zinaa,” anasema Dk
Mosha.
Takwimu hizo ni zile zilizopatikana kwa watu waliokwenda kufanyiwa uchunguzi katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Dk
Mosha anasema kuwa wanaume ndiyo huathiriwa zaidi na saratani ya mdomo
ambapo kwa hapa nchini, asilimia 53 ya wanaume waliofika MNH kwa ajili
ya vipimo, walibainika kuugua saratani hiyo, huku wanawake wakiwa ni
asilimia 47.
Utafiti kama huo
ulifanywa pia na Dk Amos Mwakigonja, mkuu wa Idara ya Patholojia katika
Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MUHAS). Dk
Mwakigonja alifanya utafiti wa saratani ya mdomo aina ya Kaposi’s
Sarcoma ambapo wagonjwa 78 walibainika na saratani hiyo kuanzia mwaka
1990 hadi 2003. “Saratani za mdomo zipo za aina nyingi na zimetofautiana
kulingana na visababishi vyake,” anasema Dk Mwakigonja.
Katika utafiti wake Dk
Mwakigonja alibaini kuwa wanawake wengi walikuwa na saratani ya mdomo
aina ya Kaposi’s Sarcoma kuliko wanaume. Hata
hivyo, utafiti huo ulionyesha kuwa asilimia 50 ya wanaume walikuwa na
saratani ya mdomo hatari zaidi (systemic) kuliko wanawake ambao ni
asilimia 37.
Mapenzi kwa mdomo husababisha maradhi. Dk Mwakigonja anasema kuwa mapenzi yoyote kwa njia ya mdomo lazima yasababishe maradhi ya zinaa iwapo mmoja ameambukizwa. Pia
anasema kwamba sampuli nyingi za wanaume wanaojihusisha na mapenzi na
wanaume wenzao (mashoga) zilibainika na saratani ya mdomo.
Utafiti huo ni sehemu ya
utafiti wa Shahada ya Uzamivu ambao ulionyesha kuwa wagonjwa wengi wa
saratani ya mdomo walikuwa ni wanaume wenye umri wa miaka kati ya 38 na
kuendelea na wanawake ni 31.
Ufatiti wa WHO Tanzania
Shirika la Afya Duniani
(WHO) pia lilifanya utafiti mwaka 2010 nchini kwa kushirikiana na Kituo
cha Taarifa za HPV, ambapo ilibainika kuwa asilimia 20 ya saratani za
koo na mdomo nchini zinasababishwa na ufanyaji wa mapenzi kwa njia ya
mdomo.
Taarifa hizo za WHO
zinaeleza kuwa wanaume 747 hugundulika na saratani ya mdomo kila mwaka
wakati wanawake 472 hubainika na saratani hiyo pia. Wakati huohuo, wanaume wanaopoteza maisha kutokana na saratani hiyo ni 444, kwa mwaka na wanawake ni 270, kwa mwaka.
Utafiti wa WHO umebaini
kuwa saratani ya mdomo inashika nafasi ya sita katika aina 24 za
saratani 24 zinazoisumbua zaidi Tanzania. Ripoti
hiyo inaeleza kuwa wanaume wanaoathirika zaidi ni wenye umri wa kati ya
miaka 15 na 55, ambao tayari wameshaanza kujihusisha na ngono.
Kama maradhi mengine ya
kuambukiza, Virusi vya HPV huambukizwa kwa urahisi zaidi kutoka kwa
wanawake kwenda kwa wanaume kuliko kutoka kwa wanaume kwenda kwa
wanawake.
Utafiti huo
uliodhaminiwa na mfuko wa Bill na Melinda Gates na Kituo cha Saratani na
Mpango wa Utafiti wa Taasisi ya ICO unaeleza kuwa mitandao ya kijamii
na picha za ngono ndiyo chanzo cha watu wengi kuiga ufanyaji wa mapenzi
ya aina hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la
The New York Times, tafiti zimefanyika na kubaini kuwa asilimia 70 ya
wagonjwa wanaobainika na saratani ya koo na mdomo duniani, husababishwa
na Virusi vya Human Pappiloma vinavyotokana na magonjwa ya zinaa. Tafiti
hizo zinaonyesha kuwa wagonjwa wengi wanaogundulika na saratani hiyo ni
wanaume wenye umri wa kati, wenye uwezo wa kifedha, wasiovuta sigara
wala siyo walevi waliokubuhu.
Utafiti huo ulibaini kuwa wanaume wapo hatarini zaidi kupata saratani ya koo inayosababishwa na Virusi vya HPV. Miaka ya 80, idadi ndogo ya watu waliougua saratani ya koo walihusishwa na maambukizi ya Virusi vya HPV. Kihistoria,
watu waliobainika na ugonjwa huo, ni wenye umri wa miaka 70 kwenda juu
ambao walikuwa ni wale walevi waliokubuhu na wavuta sigara.
Ilielezwa kuwa Virusi
vya HPV vipo kwa wingi kiasi ambacho watu wazima wanaojihusisha na ngono
ya aina yeyote ile, huweza kupata maambukizi ya zinaa hata kama siyo
saratani. Hata
hivyo ilibainishwa kuwa saratani isababishwayo na virusi vya HPV ni
rahisi kuitibu kuliko saratani ya koo isababishwayo na tumbaku au pombe
kali.
Virusi vya HPV ni nini?
Kwa jina la jumla, saratani ya koo au mdomo huitwa saratani ya kichwa na shingo. (Neck and Head Cancer). HPV
ni miongoni mwa virusi hatari zaidi duniani visababishwavyo na magonjwa
ya zinaa na vinaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili. Zipo
aina zaidi ya 120 za HPV, baadhi huweza kuzalisha usugu (warts) ambazo
si saratani katika sehemu za siri, mikononi na miguuni.
Maambukizi ya HPV hufanyika kwa urahisi, hata kwa kugusana ngozi au majimaji, huku maambukizi mengine yakisababishwa na ngono.
Virusi hatari na vinavyosababisha saratani ni HPV-16, HPV-18, HPV-31 na HPV 45. Aina
hii ya Virusi vya HPV husababisha saratani ambapo uvimbe waweza
kujitokeza kwa ndani na unaweza usionekane ukilinganisha na vivimbe
vingine vya saratani.