IMEELEZWA
kuwa ziwa Victoria liko katika hatari ya kutoweka katika ramani ya dunia
kutokana na shughuli
mbalimbalii za binadamu zinazofanywa kando ya ziwa hilo.
Mtaalamu
wa mazingira idara ya maji katika bonde la Ziwa Victoria, Wangasa Ogoma,alibainisha
hali hiyo hivi karibuni na kwamba maji
yamekuwa yakishuka kina chake kila mwaka hali inayotishia usalama wa ziwa hilo.
Ogoma
alisema shughuli hizo ni pamoja na kilimo na ujenzi unaofanywa ndani ya mita 60
kutoka katika ziwa hilo.
Nae
mkurugenzi wa mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es
salaam,Dk Julius Ningu,alisema kuna haja kwa kila mwananchi kuchukua hatua ya
kupinga shughuli hizo kwa kushirikiana na serikali.
Aliongeza
kuwa ziwa victoria ni rasilimali muhumu kwa baadhi ya nchi zinazozungukwa
na ziwa hilo hivyo linapaswa kulindwa kwa umakini zaidi.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI