Uamuzi wa kutengua
uteuzi huo wa Professa Tibaijuka,ulielezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete,alipokuwa akiongea na wazee wa Jiji la Dar Es
Salaam.
![]() |
Rais Jakaya Kikwete alisema ametengua uteuzi wake kwa Profesa Tibaijuka,baada ya kukiuka Maadili ya Utumishi wa Umma kwa kupokea Shilingi Bilioni 1.6 kati ya Shilingi Bilioni 306 zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
“Unaamka asubuhi
na kukuta akaunti yako imejaa Shilingi Bilioni 1 ama 80 haulizi,kwani MANNA hiyo? Hata MANNA hazikushuka kwenye akaunti,tumejadili nae tumemuomba atupishe
tuteue mwingine nafasi hiyo,” Alisema Rais Kikwete.
![]() |
RAIS Jakaya Kikwete akisisitiza kauli yake |
![]() |
RAIS Jakaya Kikwete akitabasamu kabla hajatoa maamuzi juu ya Profesa Anna Tibaijuka. |
![]() |
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete,akiongea kwa msisitizo. |
![]() |
WAZEE wakishangilia maamuzi ya Rais Kikwete kutengua uteuzi wa Professa Tibaijuka. |
Baada ya Rais Kikwete kutangaza maamuzi hayo
ukumbi uliripuka kwa shangwe na nderemo,huku akieleza kuhusu suala la Waziri wa
Nishati na Madini,Professa Sospeter Muhongo bado lipo kwenye uchunguzi sambamba
na Katibu wa Wizara hiyo,Eliakim Maswi,na maamuzi yao yatatangazwa baada ya
uchunguzi kukamilika.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI