Sunday, December 21, 2014

TATIZO LA MFUMUKO WA BEI KAHAMA

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO



IMEELEZWA kuwa uhaba wa upatikanaji bidhaa za biashara kutoka ndani ya wilaya Kahama mkoani Shinyanga umechangia kwa kasi suala la mfumuko wa bei ya
bidhaa wilayani humo.

Hayo yalisemwa na Katibu wa soko kuu mjini Kahama Waziri Nyalubanda katika mahojiano na gazeti hili tando yaliyofanyika ofisini kwake,ambapo alibainisha kuwa bidhaa nyingi kutoka nje ya wilaya zinasababisha kuwepo kwa mfumuko wa bei.
 



Nyalubanda aliongeza kuwa bidhaa nyingi za kibiashara hususani vyakula vimekuwa vikitoka nje ya wilaya na hata mkoa kwa ujumla jambo linalopelekea bei kupanda kutokana na gharama za usafirishaji kwa wafanyabiashara.

Kwa takwimu fupi ya bei ya mchele kwa kilo ni kati ya shilingi1800 mpaka 2000 kilo ya maharage ni shilingi 2000 Dengu ni shilingi 1800,na bidhaa zinginezo jambo ambalo kwa wenye kipato cha chini inakuwa ni vigumu kupata huduma.

Hata hivyo alisema taratibu za uongozi wa soko na serikali wakishirikiana na wafanyabiashara ni kuboresha mzunguko wa bidhaa sokoni hapo jambo ambalo litatoa unafuu wa gharama kwa wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI