KAMANDA wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilayani Kahama,Elias Kuandikwa amewakumbusha wazazi na walezi,kuwa mstari wa Mbele kupigania elimu bora kwa watoto wao hatua itakayosaidia familia nyingi kuzinusuru na wimbi la umaskini nchini.
 
Kuandikwa,alisema hayo wakati wa uzinduzi wa shule ya awali na Msingi ya Southland iliyopo Nyahanga, ambapo alikumbusha msingi wa elimu bora kwa mwanafunzi unaanzia ngazi ya familia.

Alisema wazazi ama walezi ni budi kuwapeleka vijana wao shule sambamba na kuwajengea mazingira rafiki katika masomo yao kuanzia ngazi ya awali hatua itakayosaidia kuboresha elimu na kuwafanya wanafunzi wanapohitimu kuwa wameelimika na kuwa chachu ya maendeleo katika familia zao na taifa kwa ujumla.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo,Radhaman Salim,alisema shule hiyoyenye wanafunzi 71 kati yake watatu ni yatima ambao wanasomeshwa na mfuko wa shule hiyo, iliyoanzishwa mwaka 2011 ikiwa na wanafunzi sita na walimu wawili,tayari imekamilisha usajili wake na imedhamiria kutoa kiwango bora cha elimu kwa vijana watakaosoma shuleni hapo.ika, huku mfuko wa shule hiyo ukisomesha wanafunzi watatu ambao ni yatima.

Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo,Paul Ntelya,alisema suala la elimu ni muhimu sehemu yoyote duniani na kwa kutambua hilo kamati yake imepanga mikakati ya kuifanya shule hiyo inatoa elimu bora kwa kuhakikisha inashirikiana na wazazi pia wadau mbalimbali kuhakikisha wanainua kiwango cha taaluma katika shule hiyo.


Awali wakisoma risala ya wanafunzi wa shule hiyo iliyosomwa na mwanafunzi Leticia Jackson ilieleza wajibu wa wazazi kushiriki kikamilifu katika suala la kuchangia shughuli na miradi ya shule ili kuboresha miundombinu ya shule hali itakayosaidia kuwaweka katika mazingira mazuri yatakayowezesha kusoma kwa umakini na kufanya vyema katika masomo yao.