BAADHI
ya madiwani katika Halmashauri ya wilaya
ya Chato,mkoani Geita wameiomba serikali kufanya
uchunguzi katika Halmashauri
hiyo ili kufahamu kiini cha kuharibika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita
nchini.
Kauli hiyo ilitolewa kwa nyakati tofauti na madiwani hao,huku wengi
wao wakitaka waziri ofisi ya waziri mkuu serikali za mitaa na tawala za
mikoa TAMISEMI,Hawa Ghasia kumchukulia hatua haraka mkurugenzi wao Clement
Belege
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ilemela Ismail Luge alisema Mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo ameharibu uchaguzi kwa kushindwa kuchapisha karatasi za
kupigia kura wajumbe na badala yake wananchi walipiga kwa kuandika majina
kinyume na taratibu
Luge alisema hali hiyo imefanya zoezi kuwa
gumu kwa wananchi ambao hawajui kuandika hali ambayo kwa kawaida majina
huchapwa kwenye karatasi hiyo ambayo wananchi huweka vema kwa mtu wanayemtaka
hali ambayo mkurugenzi huyo hakufanya hivyo
Kwa upande wake Belege alipotakiwa kuzungumzia
hali hiyo alisema swala hilo haliwezi kuzungumzwa kwa ufupi bali linahitaji
Maelezo marefu juu ya taratibu zilizotumika kuchapisha karatasi hizo
Madiwani
wengine wanaotaka Ghasia amchukulie hatua mkurugenzi huyo ni Eramu
Lubagola wa kata ya Bwela Stela Kiwanuko wa kata ya Kachwamba Abel Chamwanda wa
kata ya Makurugusi pamoja na Marco Maduka wa kata ya Mganza wanaodai kwa pamoja
mkurugenzi huyo amevuruga uchaguzi huo.
Chanzo cha habari ni
Shija Felician,Chato.
KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI